RAIS wa Klabu ya Yanga na Mwenyekiti wa Shirikisho la Vilabu Afrika (ACA), ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya Mashindano ya Vilabu ya FIFA. Hersi Said, ameendelea kuthibitisha nafasi yake katika maendeleo ya soka la Afrika baada ya kushiriki mazungumzo muhimu kwenye kipindi cha kimataifa cha @TransferRoom.
Katika mahojiano hayo, Hersi ameeleza kwa kina dhamira ya viongozi wa soka barani Afrika katika kujenga mifumo imara itakayohakikisha vipaji vya vijana vinalindwa, vinaendelezwa na kunufaisha vilabu pamoja na wachezaji kwa muda mrefu.
Mojawapo ya mada kuu iliyojadiliwa ni maendeleo na uhifadhi wa vipaji bora barani Afrika, ambapo amesisitiza umuhimu wa vilabu kuwekeza zaidi kwenye mifumo ya ndani badala ya kuuza vipaji mapema bila mipango endelevu.
Pia amegusi suala la kuunda njia imara kutoka shule na akademi za kufundisha mpira hadi timu za kwanza za vilabu, ameeleza kuwa mafanikio ya soka la kisasa yanategemea sana uwepo wa daraja linalowawezesha vijana kupanda hatua kwa hatua kwa misingi ya kitaalamu.
Hersi aliongeza kuwa kuwepo kwa miundombinu bora na sera sahihi kutawasaidia wachezaji vijana kupata mazingira salama ya kukua kiakili, kimwili na kiufundi kabla ya kukutana na changamoto za soka la ushindani wa juu.
Katika mjadala huo, amezungumzi pia njia za kuongeza thamani ya uhamisho wa wachezaji wa Afrika, ameeleza kuwa maandalizi sahihi na mikataba yenye tija itaongeza heshima na mapato kwa vilabu vya bara hili.
Kwa ujumla, ushiriki wa Hersi kwenye jukwaa la @TransferRoom umeonyesha wazi dira ya soka la Afrika linalojitegemea, lenye mifumo imara na lenye uwezo wa kufungua fursa kubwa za kimataifa kwa wachezaji na vilabu vyake.
The post HERSI AIBUA DIRA YA SOKA LA AFRIKA appeared first on Soka La Bongo.






