SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeufungia uwanja wa KMC Complex uliopo Dar es Salaam kutumika kwa michezo ya Ligi, baada ya kubaini kuwa haujakidhi vigezo vya kikanuni na masharti ya mpira wa miguu.
Kwa mujibu wa TFF, miundombinu ya uwanja huo imeonekana kutokukidhi matakwa yaliyoainishwa katika Kanuni ya Leseni za Klabu, hali iliyosababisha kuchukuliwa kwa uamuzi huo ili kulinda viwango na ubora wa mashindano ya soka nchin.
Kutokana na hatua hiyo, klabu zote zinazoutumia uwanja wa KMC Complex kwa michezo yao ya nyumbani zitalazimika kutumia viwanja mbadala kwa mujibu wa Kanuni, hadi pale uwanja huo utakapofanyiwa marekebisho yanayohitajika na kukaguliwa upya na TFF kabla ya kuruhusiwa kutumika tena.
TFF imeeleza kuwa itaendelea kusimamia kwa ukaribu utekelezaji wa Kanuni hizo na kuzitaka klabu zote nchini kuwekeza katika utunzaji na uboreshaji wa miundombinu ya viwanja ili kukidhi viwango vinavyotakiwa.
Uwanja wa KMC Complex ulikuwa ukitumiwa na klabu ya Yanga kama uwanja wa nyumbani, baada ya kuhamia hapo kutoka Azam Complex uliopo Chamazi, Dar es Salaam.
The post TFF YAIFUNGIA UWANJA WA KMC COMPLEX appeared first on Soka La Bongo.





