DAR ES SALAAM: BARAZA la Madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Temeke limepitisha rasimu ya bajeti kwa mwaka wa fedha 2026/2027 yenye jumla ya Shilingi bilioni 192, ambazo zinatarajiwa kutumika katika miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo elimu, barabara, afya pamoja na mikopo kwa makundi maalumu. Rasimu hiyo ilipitishwa leo, Februari 19, 2026, jijini Dar es





