SERIKALI iko katika hatua za mwisho za kuanza upanuzi wa barabara ya Kitonga mkoani Iringa ambayo sasa itakuwa ya njia nne na yenye taa za barabarani. Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega, amesema kuwa hatua hiyo ni uamuzi wa Rais Samia Suluhu Hassan ili kupunguza foleni na kuboresha usalama wa watumiaji barabara katika njia hiyo inayotumiwa






