inaendesha warsha ya mafunzo ya siku tano kwa watumishi wa Ofisi ya
Taifa ya Ukaguzi (NAOT) kwa lengo la kuhakikisha wanaendana na
mabadiliko ya viwango vya kikaguzi vya Kimataifa katika ukaguzi wao.
Warsha
hiyo inajadili masuala muhimu kama viwango vya ukaguzi, utoaji wa
taarifa za fedha kwa uadilifu, na matumizi ya viwango vipya vya
undelezaji endelevu (sustainability) pamoja na mabadiliko ya
kiteknolojia katika fani ya uhasibu.
Akizungumza wakati wa
ufunguzi, Mkurugenzi Mtendaji wa NBAA, CPA Pius Maneno, alisema Tanzania
inaongoza katika masuala ya menejimenti ya fedha za umma kwa mujibu wa
Shirikisho la Wahasibu Duniani, ikishika nafasi ya kwanza pamoja na
Nigeria katika utumiaji wa viwango wa kimataifa vya utayarishaji wa
taarifa za fedha za umma ( IPSASs).
Aliongeza kuwa mafanikio haya
yameifanya Tanzania kuwa na uwezo wa kufundisha watumishi wa serikali
kutoka nchi jirani kama Msumbiji. “Hii ni taaluma pekee duniani
inayofanya kazi kwa niaba ya maslahi ya umma,” alieleza CPA Maneno.
Msaidizi
wa Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Isaya Jeremiah, alisema kuwa
mafunzo hayo ni muhimu kwa watumishi kwani yanalenga kuboresha utendaji
wao na kuhakikisha wanakuwa na viwango vya kimataifa katika ukaguzi wa
fedha za serikali.
Aliongeza kuwa mafunzo hayo yanaendana na
matakwa ya Bodi ya Wakaguzi ili kuhakikisha wakaguzi wanabaki kuwa
“relevant” katika taaluma yao.
Mmoja wa washiriki wa semina hiyo,
Shamimu Mshana, alieleza furaha yake kushiriki mafunzo hayo, akisema
kuwa yamekuwa na msaada mkubwa hasa wakati huu wa ukaguzi wa fedha za
umma.
“Mafunzo haya yanatupa maarifa mapya na yanatusaidia
kumwezesha Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kutoa ripoti
zenye viwango vya juu,” alisema Mshana, akibainisha kuwa mafunzo hayo ni
ya manufaa katika kazi zao za kila siku. 17:59