Mwenyekiti wa chama cha wachimbaji wadogo wa dhahabu wilaya ya Igunga, Peter Mashili akizungumza na wazazi pamoja na walezi juu ya kutowatumikisha watoto kipindi hiki wanachosubiri matokea ya darasa la saba .
Mwalimu mkuu washule ya Msingi Maendeleo ,Angelina Deogratias akipokea fedha kiasi cha shilingi milion 2.150,000 kwa ajili ya kununulia mashine ya kudurufu na kompyuta kutoka kwa Mwenyekiti wa chama cha wachimbaji wadogo wa dhahabu wilaya ya Igunga, Peter Mashili.
Wanafunzi 52 waliomaliza darasa la saba katika shule ya Msingi Maendeleo wakimsikiliza Mwenyekiti wa chama cha wachimbaji wadogo wa dhahabu wilaya ya Igunga, Peter Mashili katika mahafali yaliyofanyika jana mwilayani nzega mkoani Tabora
Na Lucas Raphael,Tabora
Wazazi na walezi wilayani Nzega mkoani Tabora wametakiwa kuachana na tabia ya kuwageuza watoto wao kuwa vitega uchumi kwenye familia bali wanatakiwa kuendelea kuwalea hadi kufikia umri wa miaka 18 na kuwasaidia kutimiza ndoto na vipawa vyao ili waweze kukua kiakili na hekima kwa manufaa yao na Taifa la .
Kauli hiyo ilitolewa na Mwenyekiti wa chama cha wachimbaji wadogo wa dhahabu wilaya ya Igunga, Peter Mashili alipokuwa akizungumza na wazazi, walezi na watoto waliomaliza darasa la saba mwaka huu katika shule ya msingi Maendeleo wilayani Nzega mkoani hapa.
Alisema wazazi na walezi wanatakiwa kuwalea watoto wao kwa kufuata maadili ya kitanzana na kuacha tabia ya kuwafanya vitega uchumi wa familia jambo ambalo ni aibu .
Mwenyekiti huyo alibainisha kwamba katika kipindi ambacho wanasubiri matokeo ya kujiunga na kidato cha kwanza , kila mzazi jukumu lake liwe ni kuhakikisha wanaendeleza malezi na maadili mema .
“Wazazi na walezi muendelee kuwalea watoto wetu katika kipindi hiki ambacho wanasubiri matokeo yao kwani wanapaswa kusimamiwa ili kuendelea kuwajenga kimaadili ili wasisumbuliwe na watoto wasio na tabia njema mitaani.”Alisema
Alieleza kwamba wazazi wanawajibu mkubwa wa kutunza watoto kwa kila kitu kinachojulikana ni malezi ya baba ,mama kwa mtoto wao hasa kipindi hiki cha kusubiri matokeo na kuweza kujinga na kidato cha kwanza.
Mashili alisema kwamba watoto wanandoto zao hivyo ni muhimu wazazi kusimamia ndoto hizo ili ziweze kuwafikisha kule wanakopaswa kufika.
“Hakuna sehemu yoyote duniani mtu yoyote anaweza kuishi bila ya kuwa na ndogo hivyo ni muhimu kila mzazi kusimamia ndogo za watoto ili baadaye waweze kujenga taifa lililo bora.” Alisema Mashili.
Hata hivyo mwalimu mkuu wa shule ya Msingi Maendeleo ,Angelina Deogratias ,alisema kwamba wanafunzi wanaohitimu darasa la saba ni 52 na kwa jitihada za walimu kufundisha wanategemea watoto wote kuendelea na kidato cha kwanza mwakani .
Aidha uongozi wa shule hiyo waliomba kupatiwa mashine ya kudurufu, kompyuta au kinakilishi kwa ajili ya kudurufu mitihani kwa ajili ya wanafaunzi wa shule hiyo.