Waziri wa elimu Sayansi na Teknolojia nchini Prof.Aldof Mkenda amezindua nyumba ya mwalimu shule sekondari Lubonde wilayani Ludewa mkoani Njombe ambayo imegharimu zaidi ya mil 97 katika ujenzi wake.
Wakati akizindua Prof Mkenda amesema serikali ya mama Samia imedhamiria kufanya mageuzi katika sekta ya elimu kwa kujenga na kuboresha miundombinu kote nchini na kisha kuondoka na ombi la ujenzi wa mabweni shuleni hapo.
Awali diwani wa kata ya Lubonde Edger mtitu amesema kitendo cha serikali kujenga shule ya sekondari katika kata hiyo changa kimeondoa changamoto ya watoto kufata elimu umbali mrefu na kisha kueleza kiu ya wananchi kuona shule hiyo inakuwa na mabweni ya wanafunzi wote na kuomba serikali kuona namna ya kuwasaidia huku mbunge wa Ludewa Joseph Kamonga akitumia fursa hiyo kuomba walimu wa masomo ya sayansi.
Kwa upande wake mkuu wa shule ya sekondari Lubonde Willy Chaula amesema wametekeleza mradi wa nyumba ya walimu kwa kutumia fedha ya mradi wa kuboresha elimu wa SEQUID ambapo kiasi cha mil 100 kilitolewa kwa ajili ya ujenzi wake.