Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Kamal Group, Sameer Gupta akizungumza na ugeni wa Balozi wa Tanzania nchini Japani na TIC mara baada ya kutembelea eneo kongani la Viwanda kwa Wajapan.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Kamal Group, Sameer Gupta na Mkurugenzi Mtendaji wa TIC, Gilead Teri wakipanda mti katika walipofika eneo la Viwanda kwaajili ya Wajapani kuja kuwekeza hapa nchini.
Balozi wa Tanzania nchini Japan, Baraka Luvanda akizungumza mara baada walipofika katika eneo kongani la viwanda lililopo Kerege, Bagamoyo Mkoani Pwani kwaajili ya Wajapani kuuja kuwekeza.
Balozi wa Japan nchini Tanzania, Misawa Yasushi na Balozi wa Tanzania nchini Japan, Baraka Luvanda wakipanda mti wakishuhudiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Kamal Group, Sameer Gupta pamoja na watendaji wengine wa Kiwanda cha Kamal.
KUTOKANA na Mapinduzi ya Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan baada ya kuzindua kamati ya kitaifa ya kufanya mapitio ya maboresho ya mifumo ya kodi, Kituo cha Uwekezaji Tanzania(TIC) kinawahakikishia wawekezaji wa ndani na wa nje kufanya kazi na biashara kwa uhuru.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa TIC, Gilead Teri mara baada ya kufika katika eneo la kiwanda cha Kamal kilichopo Kerege Bagamoyo mkoa wa Pwani wakati walipotembelea kiwanda hicho kwaajili ya kuangalia eneo ambalo limetolewa kwa wa Mkurugenzi wa Kamal kwaajili ya Uwekezaji wa Wajapan.
“Wawekezaji wa nje wanaoshirikiana na watanzania tutaendelea kuwasaidiwa ili kuhakikisha kwamba uwekezaji unakua na kuongeza ajira, Serikali inapata kodi, zinapatikana fedha za kigeni, tunapata teknolojia mpya na za kisasa kwenye nchi na ndipo uchumi wetu unapokua, kwahiyo ni jambo la kujivunia na tanzania ya kesho tunaiona ikiwa njema na nzuri zaidi kuliko tuliyonayo leo.” Amesema Teri
Akizungumzia kuhusiana na sekta zinazoongoza kusajiliwa Teri amesema kuwa ni Sekta ya Viwanda inaongoza kwa ukukuaji, kuna Viwanda vingi vimesajiliwa katika miaka mitatu ya Rais Dkt. Samia kati ya Januari na Machi, 2024.
Amesema kuwa TIC imesajili miradi 109 ya viwanda pekee katika kipindi hicho ikiwa ni wastani wa kiwanda kimoja kila siku kilichosajiliwa kwa miezi mitatu ya mwanzo.
Amesema maboresho ya mifumo ya kodi itakapokamilika hakuna nchi Afrika itakayokuwa bora kuwekeza zaidi ya Tanzania, kwa sababu maeneo mengine yote tumeshayafanyia kazi. “Tumesha weka sheria za majadiliano kati ya serikali na sekta binafsi, uhuru wa mahakama, uwezo wa wafanyabishara kufanya biashara kwa uhuru pale watakapotofautiana na kuweza kushtakiana na kupata suluhisho hapa hapa nchini.”
Teri ameeleza kuwa TIC wameboresha utendaji kazi kwaajili ya kuharakisha upatikanaji wa vibali, kuwahudumia wawekezaji wanapokuja na kufanya biashara zao hapa nchini.
Pia eneo pekee lililokuwa limebaki na kulisuka vizuri ni hili la mifumo ya kodi likikamilika tunakuwa ni nchi nadhifu ambayo hakuna mtu mwingine yeyote ambaye anaweza kusema kunanchini nyingie Afrika ambayo ni bora kwaajili ya Uwekezaji zaidi ya Tanzania.
Akizungunzia sekta inayokuwa na wawekezaji wengi ni Sekta ni Ujenzi hii ni kwa upande wa ujenzi wa makazi pamoja na majengo ya kibiashara, Sekta ya Uchukuzi, hii ni Magari, Maroli pia sekta ya uhifadhi kwaajili ya bidhaa za kilimo pamoja na bidhaa za viwandani, Utalii na Kilimo.
Amesema kuwa matarajio ni kuona sekta nyingine pia zitaendelea kukua kwa kila uchwao.
“Ukuaji wa Uchumi wa Tanzania ni ukuaji mzuri na unakua kwa kasi kadri siku zinavyozidi kwenda tunaamini tutazidi kukua na kuwa vizuri zaidi kwa sababu mambo ya msingi ikiwemo maboresho ya mazingira ya uwekezaji na maboresho ya kodi yanafanya mazingira yawe rahisi sana kwa mtanzania yeyote anayetaka kunzisha uwekezaji hana sababu ya kutokuanzisha kwani mazingira ya serikali ya awamu ya sita ni mazuri, kazi kwake tuu kuanza kupata faida na kukuza kipato cha kwake na cha nchi kwa ujumla.” Ameeleza Teri
Teri amesema serikali ya awamu ya sita imeliweka mipango ya jinsi ya kuvutia uwekezaji kwa kufanya maboresho ya sheria ya EPZ na sheria ya uwekezaji ya 2022 ambayo inatoa vivutio vya kikodi ambavyo ni nafuu ambavyo serikali inavitoa kwa mtanzai anayetaka kuanzisha biashara aweze kukua kwa unafuu zaidi.
Kwa Upande wa Balozi wa Tanzania nchini Japan, Baraka Luvanda amesema kuwa namba hazidanganyi kwa kuja na Watu 60 wanatarajia wanapata wawekezaji wengi kutoka Japan ambao wamebobea katika maeneo mbalimbali.
Amesema kuwa tutarajie kupata wawekezaji katika maeneo ya Miundombinu ya barabara, ujenzi wa madaraja, bandari, Viwanja vya ndege, miundombinu ya Afya na miundombinu ya maji.
Akizungumza walipofika katika eneo kongani la Viwanda lililopo katika kiwanda cha Kamal kilichopo Kerege mkoani Bagamoyo mkoani pwani, Balozi Luvanda amesema kuwa uwekezaji huo tunautarajia ni ule wa ubia kwa kuungana na watanzania kutoka sekta mbalimbali pia wanaweza kutumia fedha zao na utaalaam wao.
Licha ya hayo Balozi Luvanda ameeleza kuwa tayari kwa hapa nchini kuna kampuni 51 za uwekezaji ambazo tayari zimeshawekeza.
Kwa Upande wa Balozi wa Japan nchini Tanzania, Misawa Yasushi amesema kuwa Tanzania ni nchi ya ahadi.
“Nina uhakika kuwa Tanzania kupitia uwekezaji katika viwanda itakuwa na uchumi imara zaidi hapo baadae.”
Pia anatumaini kuwa kampuni za Japan zitakuja kuwekeza nchini Tanzania na haitachukua muda mwingi Wajapan kuchukua fursa ya kuja kuwekeza Tanzania na kudumisha ushirikiano uliopo wa miongo kadhaa kati ya Tanzania na Japan.