Takriban Wapalestina 50 waliuawa na makumi ya wengine kujeruhiwa katika mashambulizi ya Israel Jumatatu katika maeneo kadhaa ya Ukanda wa Gaza, kulingana na vyanzo vya afya.
Jeshi la Israel liliendelea na mashambulizi yake katika maeneo ya kaskazini, kusini na katikati mwa eneo lililozingirwa katika kumbukumbu ya mwaka wa kwanza wa vita vya Israel na Hamas.
Duru za afya zilisema Wapalestina watatu waliuawa katika shambulio la ndege isiyokuwa na rubani (UAV) kwenye hema karibu na Msikiti wa Al-Furqan katika kambi ya wakimbizi ya Bureij katikati mwa Gaza.
Wapalestina watano waliuawa na 18 kujeruhiwa katika mashambulizi mawili ya anga katika maeneo mengine katika kambi hiyo.
Wapalestina wengine 16 waliuawa katika mashambulizi tofauti mashariki na magharibi mwa Khan Younis.
Katika mji wa Rafah, Wapalestina wanane waliuawa katika shambulio la ndege za kivita za Israel zilizolenga nyumba moja katika eneo la Miraj, na Mpalestina mmoja aliuawa katika shambulio katika eneo la Khirbet al-Ades.
The post Wapalestina 50 wauawa katika mashambulizi ya Israel katika kumbukumbu ya mwaka mmoja wa vita visivyokoma first appeared on Millard Ayo.