Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, DKt. Hussein Ali Mwinyi, amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan Kwa kuchangia kuongeza Idadi ya Watalii na Ongezeko la Pato la Taifa baada ya kushiriki Katika Filamu ya Royal Tour.
Rais Mwinyi ameyasema hayo leo Oktoba 11, 2024 wakati akifungua Onesho la 8 la Utalii la Kimataifa la Swahili (8th edition of the swahili international tourism expo – S!TE 2024) katika ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es salaam ambalo limewakutanisha Wadau wa UTALII, Wawekezaji, Waoneshaji na Wanunuzi wa bidhaa za Utalii.
Rais Mwinyi ameipongeza Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii na Bodi ya Utalii Kwa jitihada wanazozifanya kuhakikisha Mapato yanapatikana Katika Sekta hiyo Kwa kipindi Cha muda mfupi.
“Kutokana na juhudi hizo za Mheshimiwa Rais Dkt. Samia, idadi ya watalii wa kimataifa wanaotembelea Nchi yetu imekua kwa kasi sambamba na ongezeko la mapato yatokanayo na sekta ya utalii” alisema Dkt. Mwinyi.
Aliongeza Kwa kusema hadi kufikia mwezi Agosti, 2024 Tanzania imepokea jumla ya watalii wa kimataifa 2,026,378 ikiwa ni takwimu za juu kabisa kuwahi kufikiwa katika historia ya Nchi yetu. Pia, mapato yatokanayo na sekta ya utalii yamefikia Dola za Marekani bilioni 3.5”. amesema Dkt. Mwinyi.
Hata hivyo, Rais Mwinyi amesema kuwa mafanikio hayo yamewezesha nchi yetu kutambuliwa kimataifa na kupata tuzo mbalimbali ambapo taarifa iliyotolewa mwezi Septemba, 2024 na Shirika la Utalii Duniani (UN Tourism – World Tourism Barometer) ambapo inaonesha kuwa, Tanzania imeshika nafasi ya 6 Duniani na ya kwanza Barani Afrika kwa kuwa na ongezeko kubwa la Watalii.
Kwa Upande wake,Waziri wa Maliasili, Balozi, Dokta Pindi Chana na amemshukuru Rais Mwinyi na kuomba afikishe salama Kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.