Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza na Kamati Kuu inayosimamia kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru zitakazofanyika Uwanja wa CCM Kirumba.
Na: Mwandishi Wetu – MWANZA
WAZIRI Mkuu, mhe. Kassim Majaliwa ameridhishwa na maandalizi ya maadhimisho ya kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru ambayo yatafanyika mkoani Mwanza, Oktoba 14, 2024.
Amesema hayo leo Oktoba 13, 2024 wakati akikagua maandalizi hayo ambayo yatafanyika katika uwanja wa CCM Kirumba, Jijini Mwanza.
“Nimeridhishwa na maandalizi na niwapongeze kwa kukamilisha shughuli zote za maandalizi haya,” amesema
Awali akitoa taarifa ya maandalizi hayo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete amesema maandalizi yamekamilika na hamasa kubwa imefanywa na Mkoa wa Mwanza katika kuhamasisha wananchi kushiriki kwa wingi katika maadhimisho hayo ambayo mgeni rasmi anatakuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza na Kamati Kuu inayosimamia kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru zitakazofanyika Uwanja wa CCM Kirumba.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete akiwasilisha taarifa ya maandalizi ya sherehe za kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru kwa Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa alipokutana na Kamati ya maandalizi hayo katika uwanja CCM Kirumba kwa ajili ya kukagua maandalizi hayo yatakayofanyika jijini Mwanza.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete alipowasili kwenye uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza leo Oktoba 13, 2024 kuelekea kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru kesho tarehe 14 Oktoba, 2024.