Katika kuadhimisha kumbukizi ya miaka 25 ya kifo cha Baba wa Taifa mwalimu julias kambalage Nyerere watumishi wa shirika la umeme Tànesco MKoa wa Lindi wametembelea na kutoa mahitaji maalumu katika kituo cha kulelea watoto cha loving heart.
Msaada uliotolewa kituoni hapo ni pamoja na unga , mchele, mafuta ya kupikia, sabuni juice,Sukari, sufulia pamoja na jiko janja la kupikia la umeme.
Akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada huo Meneja wa Tànesco MKoa wa Lindi Athumani Jumbe amesema wameamua kutembelea kituo hicho ili kuwapa faraja watoto wanaoishi Katika kituo hicho pamoja na walezi wao.
Afisa mahusiano na huduma kwa wateja wa shirika hilo MKoa wa Lindi Robert Fred amesema wameona kuwakabudhi jiko janja la umeme ili kuwarahisishia shughuli zao za mapishi ikiwa sambamba na kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Rais Samia za kuhamasisha matumizi ya nishati Safi.
Joyce Makajula ni malezi wa kituo hicho cha loving heart amelishukuru Shirika hilo la Tànesco kwa kukukumbuka kituo hicho na kwamba jiko walilolitoa litawasaidia kurahisisha shughuli zao za upishi