Mkuu wa Wilaya ya Bahi Rebecca Nsemwa ameitaka Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) kuwachunguza watumishi wa umma wa wilaya hiyo akiwemo askari Polisi wa kata ya ya Chipanga kwa tuhuma za kushiriki kuficha ushahidi wa kifo cha Lucia Ilamba (30) mama mjamzito mkazi wa Chipanga wilaya ya Bahi mkoa wa Dodoma
Maagizo ya DC Nsemwa yametoka kufuatia utata wa mazingira ya kifo cha marehemu Lucia anaedaiwa kufariki Oktoba 25,2024 na mwili wake kukutwa chini na kamba shingoni ukionesha kujinyonga jambo ambalo limeleta taharuki wilayani.
“Huu ni ukatili uliopiliza huu ni ukosefu wa maadili ulipitiliza wewe mtaalamu wa afya unaenda kufanya postmortem bila fomu huandiki popote nakuliza huna ulipoandika,naelekeza mkuu wa takukuru naomba uwachunguze masunga na mtaalamu wetu wa kituo cha afanya kwasababu hawajafuata taratibu katika kifo hiki” Rebecca Nsemwa DC BAHI
“Nashangazwa na baadhi ya watumishi na wananchi kutokuwa na ushirikiano na ngazi ya Serikali kutokana na wataalamu wa ngazi ya Kijiji kutotoa taarifa zinazotokea katika Kijiji hichi wakati utaratibu wa kila ngazi na idara ya wataalamu inajulikana” DC Nsemwa.
The post DC Bahi aitaka TAKUKURU kuwachunguza watumishi wa umma wa wilaya hiyo akiwemo askari Polisi wa kata ya ya Chipanga first appeared on Millard Ayo.