KAMISHNA Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Yusuph Mwenda amesema kuanzia January mwakani itakuja na mpango wa kuwekeza katika mfumo wa kodi za ndani (IDRAS) ambao utasaidia kuondoa changamoto za migogoro ya kikodi na kurahisisha ukusanyaji wake.
Kamishna aliyasema hayo jana katika kikao maalumu kilichoandaliwa na mamlaka hiyo kwa kushirikiana na Benki Kuu ya Tanzania (BOT) kilicholengea kujadili namna bora ya kukusanya kodi na kuondoa vikwazo katika taasisi za kifedha.
Mwenda alisistiza lengo la kikao hicho ni kujadili namna ya kukuza biashara kwa taasisi za kifedha na kurahisisha upatikanji wa kodi ambayo ndio msingi wa maendeleo ya nchi.
Alisema hatua ya mwisho kwa watakao kuwa wakaidi kulipa kodi watatumia mawakala wa benki japo zipo njia mabazo watazitumia awali kabla ya kufikia hatua hiyo.
Alisema TRA lazima tuwaite tukae nao tuwasikilize na tuwape fursa ya kulipa kidogo kidogo na kuongeza kuwa lazima tuwaandikie barua ya nia ya kutumia Benki kama mawakala japo njia hiyo haiwezi kutumika mpaka mimi nijiridhishe” alifafanua
Hata hivyo alisistiza hatamani kufikia katika hatua hiyo kwa kuwa njia hizo ni ndefu na kwamba atahakikisha wanatumia njia nyingine kufikia suluhu.
“Tutakaa nao tutajenga mahusiano ili tukubaliane namna bora ya wao kulipa madeni na kuwashauri waendele kutumia huduma za kibenki kwakuwa itawaweka katika nafasi ya kupata mikopo mikubwa kwaajili kuendesha biashara zao.
Naye Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Emmanuel Tutuba alisema la majadiliano hayo ni ya kuangalia namna ya kuboresha mazingira ya kufanya biashara na kuwezesha taasisi za kifedha kusaidia shughuli za kibiashara ili kuongeza ukusanyaji wa kodi.
Alisema benki ni miongoni mwa taasisi zinazolipa kodi kubwa na inatumika kama mawakala wa kukusanya kodi na kutunza fedha za walipakodi na kwamba kutokana na umhuimu huo kuna haja ya kuwa kitu kimoja ili kuboresha mazingira hayo.
Kwa upande wake Mwakilishi wa Umoja wa Mabenki nchi(TBA)ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) Theobald Sabi alisema majadiliano hayo ni hatua nzuri katika sekta nzima ya fedha.
Alisema hatua hizo pia zitawapa wateja wao morali ya kuendeela kutumia kuweka fedha benki huku akisifu zitaleta matokeo chanya na kuwapa wateja imani kubwa ya kutumia mifumo rasmi Katika biashara.