ASKOFU wa makanisa ya International Evangelism Dk .Eliud Issagya akizungumza na wahitimu hao kwenye mahafali hayo wilayani Arumeru mkoani Arusha
…………..
Happy Lazaro, Arusha.
ASKOFU wa makanisa ya International Evangelism Dk .Eliud Issagya amewataka watanzania nchini kuendelea kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwani ni haki ya kila mtanzania kufanya hivyo .
Ameyasema hayo mkoani Arusha wakati akizungumza katika mahafali ya 12 ya kidato cha nne katika shule ya sekondari Hebron na mahafali ya 15 ya shule ya msingi Sluys Anderson wilayani Arumeru mkoani Arusha .
Issagya amesema kuwa, ni haki ya kila mtanzania kujitokeza kujiandikisha ili wawe na haki ya kupiga kura kuchagua kiongozi wanayemtaka kwani ni haki yao kufanya hivyo.
Aidha Askofu Issagya alituma fursa hiyo kuwataka wanafunzi hao kuenenda katika.maadili mema kama walivyolelewa vizuri shuleni hapo huku wakijuepusha na vitendo viovu ambavyo vitawaharibia maisha yao ya baadaye.
“Na nyie wazazi hakikisheni mnaangalia namna mnavyowalea watoto wenu na mhakikishe mnawaeleza ukweli kuwa maisha sio lelemama bila kuwa na elimu hawawawezi kutoboa maisha kabisa”amesema Askofu Issagya.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa shule hizo,Godwin Selembo amesema kuwa, shule hizo zimekuwa zikifanya vizuri katika matokeo ya mitihani mbalimbali kutokana na kuwepo kwa waalimu bora na waliobobea katika masomo mbalimbali.
Amesema kuwa, shule hiyo imeendelea kufanya vizuri kwenye mitihani ya Taifa kidato cha pili,nne na kidato cha sita ,ambapo amesema shule ina bustani nzuri ya mboga kwa ajili ya kuboresha chakula cha wanafunzi na kuwawezesha wanafunzi kupata mafunzo kwa vitendo .
Kwa upande wake Mkuu msaidizi wa shule ya sekondari Hebron ,Mbarikiwa Mensa amesema kuwa shule hiyo imefanikiwa kuwa na mabweni mazuri kwa ajili ya wanafunzi wa kike na wa kiume hivyo kuwafanya wanafunzi kuepuka vishawishi vya njiani na nyumbani pia.
Aidha ametaja changamoto zinazowakabili kuwa ni pamoja na usafiri wa shule kwani ni changamoto kubwa kwa ajili ya wanafunzi wanapougua kwani huwa wanakosa usafiri wa kuwapeleka hospitali.
Ameongeza kuwa ,wanakabiliwa na changamoto ya ubovu wa barabara na njia za kuingilia shuleni kwani imekuwa changamoto kubwa kwa wanafunzi na ,wafanyakazi wa shule mbalimbali wanaofika shuleni hasa kipindi cha mvua.
“Tuna changamoto nyingine ya kutokuwa na bwalo la chakula kwakili ya wanafunzi ambapo hadi sasa hivi tumeshasimamisha jengo na kuweka paa ila kwa sasa tumekwama kuweka madirisha na sakafu na inahitajika kiasi cha shs 25 milioni “amesema Mensa.
Nao baadhi ya wahitimu walisema kuwa ,wanashukuru shule hiyo kwa namna ambavyo imeweza kuwafundisha masomo ambayo mwisho wa siku wataweza kujiajiri .