Na Prisca Libaga Arusha
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Kanda ya Kaskazini kwa kushirikiana na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Longido tarehe 18.10.2024 imetoa elimu kinga dhidi ya tatizo la dawa za kulevya kwa wanafunzi 600 wa Shule ya Msingi Longido na Wanafunzi 180 wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Samia iliyopo wilayani Longido katika Mkoa wa Arusha.
Wanafunzi hao walipewa elimu juu ya madhara yanayotokana na matumizi ya dawa za kulevya na kuhimizwa kuepuka mazingira hatarishi na makundi ambayo sio sahihi ili kujikinga kujihusisha na matumizi ya dawa za kulevya.
Pia, walihimizwa kutoa taarifa za wahalifu wa dawa za kulevya kwa kupiga namba ya simu ya bure ya 119.