Naibu waziri wa Kilimo David Silinde akizungumza kwenye Maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Vyama vya Ushirika wa Akiba na Mikopo Duniani yanayofanyika Jinini Mwanza.
Mrajis msaidizi vyama vya kifedha Tanzania, Josephat Kisamalala akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Kilimo David Silinde kwenye maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Vyama vya Ushirika wa Akiba na Mikopo Duniani yanayofanyika Jijini Mwanza.
Mrajis wa Vyama vya Ushirika Tanzania Bara Dkt.Benson Ndiege akizungumza kwenye Maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Vyama vya Ushirika wa Akiba na Mikopo Duniani Mkoani Mwanza
…………
Na Hellen Mtereko, Mwanza
Vyama vya Ushirika wa Akiba na Mikopo nchini (SACCOS) vimelalamikia tabia ya baadhi ya waajiri kuchelewesha fedha za michango ya wanachama ambazo zinakatwa kutoka kwenye mishahara yao hali inayokwamisha shughuli za kiutendaji hususani katika kuwahudumia wanachama wake.
Hayo yamebainishwa Leo Octoba 21, 2024 Jijini Mwanza na Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika wa Akiba na Mikopo (SCCULT), Aziza Mshana wakati akizungumza kwenye maadhimisho ya siku ya kimataifa ya vyama vya ushirika Duniani ambayo kitaifa yanafanyika mkoani humo ,ambapo pamoja na mambo mengine amesema hali hiyo imekuwa kikwazo kwa jumuiya ya ushirika.
Akizungumza mbele ya Naibu Waziri wa Kilimo David Silinde aliyekuwa mgeni rasmi katika maadhimisho hayo Mshana amesema vyama vya ushirika vinapitia changanoto nyingi lakini hii ya kucheleweshwa kwa fedha hizo kumekuwa na athari kubwa zaidi hasa ikizingatiwa kuwa Saccos haziruhusiwi kukusanya amana kutoka kwa umma na hivyo kukosa vyanzo vingine vya kupata fedha za kuendesha shughuli zao.
“Fedha hizo hucheleweshwa kwa kipindi kirefu hadi miezi mitano ,hii inaleta kadhia kubwa kwenye utoaji wa huduma,ukizingatia saccos hizi zinatumia fedha za wanachama wake tu na haturuhusiwi kukusanya amana kutoka kwa umma” amesema Mshana
Aidha Naibu Waziri wa Kilimo, David Silinde akifungua maadhimisho hayo licha ya kueleza kusikitishwa kwake na ucheleweshaji wa fedha hizo amekemea kitendo hicho nakusema kuwa fedha hizo sio mali ya mwajiri bali ni mali ya mwajiriwa ambae ni mwanachama wa Saccos na malimbikizo hayo yamekuwa yakikosesha ukwasi SACCOS na nguvu ya kuhudumia wanachama wake kwa wakati.
“Kwanza nikemee kwa nguvu mambo haya kwasababu jambo hili halikubaliki na naomba waajiri waliache mara Moja, kanuni za huduma ndogo za fedha kanuni ya 88 imeelekezaSacoss na waajiro kusaini makubaliano ambayo yayasaidia kuo doa changmoto hii, lakini kutomaba na uzito wa changamito hii ofisi yangu itafanya mazinguzo na wahusika wa ikiwemo na wakurugebzi wa halmashauri”, alisema Silinde
Kwa upande wake Mrajis wa Vyama vya Ushirika Tanzania Bara, Dkt. Benson Ndiege amewaasa wanaushirika wa akiba na mikopo kuendelea kuwa wabunifu ili kuweza kuwa na utoafauti wa kuwahudumia wanachama.