Na Mwandishi Wetu
WATAALAM 800 kutoka nchi 21 wamekutana jijini Dar es Salaam katika kongamano la 10 la Jotoardhi Afrika (ARGeo-C10).
Hayo yameelezwa na Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Innocent Luoga wakati akifungua mafunzo kuhusu masuala mbalimbali ya Jotoardhi kwa niaba ya Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Dk Khatibu Kazungu ikiwa ni sehemu ya programu ya siku saba za Kongamano hilo.
“Katika Kongamano hili washiriki watafaidika na masuala mbalimbali ikiwemo kupata ufahamu wa kina kuhusu maendeleo ya rasilimali za jotoardhi kupitia mazungumzo na warsha za kiufundi, kubadilishana uzoefu, kutembelea na kujifunza kwa vitendo katika maeneo ya miradi ya jotoardhi, kujadili athari za masoko ya kaboni (carbon markets) na kukuza Uwezo: Kupitia kozi fupi za kiufundi,” alisema Mhandisi Luoga
Alisema Tanzania kuwa mwenyeji wa kongamano hilo kunatokana na juhudi zinazofanywa na Serikali katika uendelezaji wa sekta ya nishati ikiwemo jotoardhi.