Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Hussein Ali Mwinyi kushoto akizungumza na Wanafunzi alipolitembelea Mdarasa Mbalimbali ya Skuli ya Sekondari ya Mkokotoni baada ya kuifungua Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Na Ali Issa Maelezo 23/10/2024
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussen Ali Mwinyi amesema Serkali imeweka miundombinu bora ya kujifunzia kwa wanafuzi ili kuwajenga vyema kulingana na maendeleo ya Teknolojia Duniani.
Ameyasema hayo leo huko Mkokotoni, Mkowa wa Kaskazini Unguja wakati waufunguzi wa skuli ya Sekondari Mkokotoni katika hafla ya maadhimisho ya miaka minane ya Serkali ya awamu ya nane.
Amesema Serkali imefanikiwa kuboresha miundombinu kwa kujenga skuli za kisasa na kuzikarabati skuli za zamani ambapo jumla ya madarasa 2,773 yenye vifaa vya kisasa yamejengwa ili kuleta maendeleo katika sekta ya elimu.
Ameongeza kuwa, Serikali imeajiri Walimu 3,600 na kuboresha maslahi ya Walimu ili kuleta ufanisi zaidi katika sekta hiyo.
“Ndugu zangu Dunia ya kisasa ni dunia inayo kwenda na teknolojia hivyo hatuwezi kubaki nyuma na ndio maana tuna mabara za kisasa zenye kumputa na ndio maana tunataka kufundisha kupitia mtandao” alisema Dkt. Mwinyi
Nae katibu mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Khamis Abdalla Saidi akitoa ripoti ya kitaalamu amesema ujenzi wa skuli hiyo ya mkokotoni ni mkakati wa kuimarisha mazingira bora ya kujifundishia kwa wanafunzi.
Amesema ujenzi huo wa ghorofa tatu umezingatia mahitaji mbalimbali ikiwemo madarasa 42 vyoo 52,ofisi ya Mwalimu mkuu, ukumbi wa mkutano, mabara mbili za sayansi, chumba TEHAMA, sehemu za kuswalia wanawake, chumba mktaba na chumba cha ushauri nasaha.
Ujenzi huo umeaza mwezi mei 2023 na umekamilika octoba na ambapo zaidi ya shilingi bilioni sita zimetumika hadi kumaliza kwake ikiwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi 1850 kwa wakati mmoja.