Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Profesa Adolf Mkenda, tarehe 23 Oktoba, 2024 ametembelea Banda la Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) kwenye maadhimisho ya nne ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa yenye kauli mbiu isemayo “Elimu ya Fedha, Msingi wa Maendeleo ya Uchumi”, yanayoendelea katika viwanja vya Ruanda Nzovwe, jijini Mbeya.
Mhe. Profesa Mkenda ameipongeza NSSF kwa kuendelea kutoa elimu ya hifadhi ya jamii kwa wananchi waliopo katika sekta binafsi na sekta isiyo rasmi. Pia, amefurahishwa na huduma zinazotolewa na NSSF katika maonesho hayo hususani huduma za kufuatilia michango kidijitali.
NSSF inashiriki maonesho haya kama mdau muhimu ambapo inatoa elimu ya hifadhi ya jamii kwa sekta binafsi na sekta isiyo rasmi, kuandikisha wanachama wapya, kusikiliza na kutatua kero za wanachama, elimu ya mifumo ya TEHAMA pamoja na kutangaza fursa za nyumba na viwanja.