………………….
Na Mariam Mtani KibitiDc.
Ikiwa ni uzinduzi na utekelezaji wa agizo la Mhe .Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kila Mkoa kuhakikisha wanamaliza migogoro ya wakulima na wafugaji, Waziri wa Ujenzi Mhe. Innocent Bashungwa amekabidhi hati za kimila 136 kwa wafugaji za Ranchi ndogo Wilaya ya Kibiti .
Akikabidhi Hati hizo kwa wafugaji wachache kwa uwakilishi wa wengine , Mhe. Bashungwa amesema kitendo hicho ni ishara tosha ya kuishi pamoja na kutegemeana.
Mara baada ya kukabidhi hati hizo ,Waziri Bashungwa amemwagiza Mkuu wa Wilaya ya Kibiti Kanali Joseph kuhakikisha hakuna mfugaji atakaelisha Mifugo yake mazao ya wakulima kwani, Serikali itataka wakulima walime kwa amani bila Mifugo kuingia mashambani ukizingatia kwa sasa kila zao ni la biashara na bei zinaimarika” Alisema.
Aidha Mratibu wa mpango wa Ranchi ndogo Dkt. Ramadhan Mwaiganju alisema hati hizo zitawezesha wafugaji kumiliki maeneo ya malisho na kuyaaendeleza kisheria na matarajio yakiwa ni kusaidia ama kumaliza migogoro ya wafugaji na na watumiaji wengine wa ardhi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa wafugaji Wilaya ya Kibiti bwana Musa Kulwa Jibunge amesema kitendo cha kupewa hati kimewafirajisha, kwani sasa wanakwenda kufuga kisasa kwa utulivu na uhakika wa Watoto wao kupata elimu tofauti na awali walivyokua wakiishi kwa kuhama hama.