Mshambulizi wa Newcastle United, Alexander Isak hana mpango wa kukubaliana na mkataba mpya ambao utafungua milango ya kuhamia Arsenal, limeripoti Daily Mail.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Uswidi kwa sasa yuko chini ya mkataba na Magpies hadi 2028, hata hivyo, ripoti hiyo inafichua kuwa majadiliano ya awali kuelekea mwisho wa msimu uliopita yalimfanya Isak kusita kukubaliana na mkataba mpya.
Sababu kuu kwa nini Isak na wawakilishi wake hawakutaka kuweka kalamu kwenye mkataba mpya ni kutokana na nia yake ya kucheza Ligi ya Mabingwa ya UEFA.
Mazungumzo hayo kuelekea mwisho wa msimu uliopita yamefikia tamati na kwamba hakuna majadiliano ya sasa juu ya kandarasi mpya, huku klabu na mchezaji wakiamini kuwa mkataba mpya hauhitajiki
Habari hizi zitakuwa za manufaa kwa Arsenal, ambao wamekuwa wakimtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25.
Ripoti hiyo inadai kuwa The Gunners “wanaweza kuwa katika nafasi ya kuweka rekodi ya Uingereza” kwa Isak, huku wababe hao wa London kaskazini wakitamani kuongeza kwenye nafasi zao za mbele. Arsenal wanahitaji mshambuliaji anayetambulika wa kutoka nje, ambaye anaweza kuwafanya The Gunners kutafuta dau la kumnunua Msweden huyo
The post Je Arsenal wanaweza kumnunua Isak baada ya kutokubali kusaini mkataba? first appeared on Millard Ayo.