Na Prisca Pances
MADAKTARI Bingwa na Wabobezi wa Saratani nchini wameupongeza Ubalozi wa India kwa kuwapa mafunzo ya namna nzuri ya kutokomeza Saratani Dunia.
Ni wazi Saratani imekuwa ni tatizo linalotesa watu wengi duniani huku Afrika ikitarajiwa kuwa na ongezeko la vifo vingi ifikapo 2040 huku Tanzania pekee ikiripoti visa vipya 40,464 kwa kila mwaka ambayo ni sawa na asilimia 70 hivyo kupitia mafunzo hayo yatasaidia kupiga hatua.
Akizungumza katika ubalozi wa India nchini Tanzania uliopo dar es salaam Leo,Oktoba29,2024 Mkurungenzi Msaidizi wa Magonjwa yasiyoambukiza, Afya ya akili na ajali kutoka Wizara ya Afya, Dk Omary Ubuguyu amesema mafunzo waliyopewa ni wazi yatasaidia kuimalisha huduma za Afya nchini na kuleta Mapinduzi chanya kwenye wizara husika.
“Ni wazi kwa sasa Saratani ya matiti na mlango wa kizazi zinaitesa jamii na nilazima watu wapate matibabu hivyo basi kama Tanzania tunashirikiana na India kwa kupeleka wagonjwa wetu kwani ni hospitali ya umma ili kuendelea kubadilishana uzoefu kwa kuangalia namna wenzetu wanavyotoa huduma katika nyanja za Upasuaji,mionzi pamoja na utoaji wa dawa hivyo mafunzo haya yameleta kitu kipya katika sekta ya afya,”alisema.
Amesema kupitia mafunzo hayo ni wazi mahusiano kati ya Tanzania na India yanaendelea kuimalika zaidi sababu wanatarajia kupeleka wanafunzi na wataalamu wengi kwa ajili ya kufanya tafiti ilikuongeza ujuzi wa kutibu tatizo ambapo atanza mtu mmoja mmoja, taasisi na baadae wizara yenye dhamani.
Naye Mkurungenzi wa Huduma za Tiba kutoka Taasisi ya Saratani Ocean Road,dk Mark Mseti amesema ilikupunguza tatizo la saratani ni vyema jamii ikapewa elimu zaidi kwani Saratani bado haieleweki kwa jamii ukilinganisha na magonjwa mengine ya kuambukiza.
“Ni vyema jambo hili likatiwa mkazo kwa kutoa elimu kwa ngazi zote sababu saratani haitambuliki hivyo ni wakati wa kufanya tafiti na kuipa jamii majibu ya tafiti kwa ueleza visababishi vya tatizo,dawa zinazotumika ili mtu anapogundua shida hiyo aweze kuwa hospital,”amesema
Amesema India na Tanzania zitashirikiana katika kutoa matibabu hapa nchini badala ya mgonjwa kusafiri kwenda India, tafiti pamoja na mafunzo kwani wataalamu hao watapata mbinu nyingi za kuzuia Saratani kupitia ukubwa wa tatizo uliopo eneo hilo kwa kupata uelewa wa kukabiliana na Saratani yeyote atakayokuwa na mgonjwa na kuokoa maisha yake.
Naibu Mkurungenzi wa hospitali ya kumbukumbu ya Tata(Mumbai),Profesa Shailesh Shrikhande amesema ushirikiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na India ndio unaitoa fursa kwao kujifunza na kubadilisha ujuzi ili kuleta maendeleo nchini.
Shrikhande ambaye pia ni kiongozi wa taasisi inayotoka Huduma ya upasuaji wa Mfumo wa mmeng’enyo wa chakula na idara ya upasuaji wa Saratani amesema katika kufanikisha hayo yote ni lazima kuwepo na miundombinu rafiki lakini pia kuendana na mabadaliko ya teknolojia hivyo itasaidia na kutokomeza Saratani dunia kote.
Mafunzo hayo yametolewa kwa madaktari na wataalamu 70 wa saratani kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili, Agha Khan na Ocean Road.