BARAZA la Mitihani lTanzania (Necta) latangaza matokeo ya
darasa la saba, ambapo mtihani ulifanyika Septemba 2024.
Akitangaza matokeo hayo jijini Dar es Salaam leo, Oktoba
29,2024, Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Dkt. Said Mohamed amesema kuwa jumla
ya watahiniwa 1,230,774 walisajiliwa kufanya Mtihani wa Kumaliza Elimu ya
Msingi wakiwemo Wasichana 666,597 sawa na asilimia 54.16% na Wavulana 564,177
sawa na 45.84. Kati ya watahiniwa waliosajiliwa, watahiniwa wenye mahitaji
maalum walikuwa 4,583 sawa na asilimia 0.37 na Kati ya watahiniwa 1,230,774
waliosajiliwa, watahiniwa 1,204,899 sawa na asilimia 97.90 walifanya mtihani
wakiwemo Wasichana 656,160 sawa na
asilimia 98.43 na Wavulana 548,739 sawa na 97.26.
BONYEZA HAPA KUANGALIA MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024.