Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania, Zanzibar (TAMWA ZNZ) kwa kushirikiana na Jumuiya ya Wanawake wenye Ulemavu Zanzibar (JUWAUZA), Jumuiya ya Wanasheria Wanawake Zanzibar (ZAFELA) na Jumuiya ya mazingira, Jinsia na Utetezi Pemba (PEGAO) tuna furaha kutangaza rasmi uzinduzi wa Tuzo ya uwiano wa kijinsia kwa Vyombo vya Habari “Media for Gender Equity Awards” yenye ujumbe unaosema “Kalamu Yangu, Mchango Wangu kwa Wanawake.” Tuzo hii itatambua vyombo vya habari na waandishi wa habari Zanzibar vinavyoandika habari za kina kuhusu mafanikio, changamoto, michango ya wanawake katika uongozi, na vinavyoshiriki kikamilifu katika kukuza usawa wa kijinsia kupitia kazi zao.
Malengo ya Tuzo
Kupitia tuzo hii, TAMWA ZNZ inalenga kuhamasisha vyombo vya habari na waandishi wa habari kuunga mkono sauti za wanawake na kukuza uandishi wa habari wenye kuzingatia usawa wa kijinsia ili kuchangia mabadiliko ya kijamii kwa kuonesha nafasi za wanawake na uwezo wao katika uongozi ili kuleta maendeleo.
Utambuzi wa vyombo vya habari:
Mara hii tuzo hizi zinalenga zaidi kutambua vyombo vya habari vyenye mtiririko mzuri wa kusaidia kuongeza wanawake katika nafasi za uongozi. Hivyo vigezo vitakavyotumika ni kuwa na sera ya kijinsia, dawati la kijinsia, zana za tathmini na ufuatiliaji wa masuala ya usawa wa kijinsia, idadi ya habari zilizoandikwa kuhusu
wanawake na uongozi na nafasi ya wanawake waandishi wa habari katika chombo cha habari. Mradi wa SWIL uliwahi kuwapa mafunzo na kusaidia vyombo vya habari
@TAMWA_Zanzibar www.tamwaznz.or.tz
11 kutoka Unguja na Pemba kuandika na kuweka kumbukumbu na kufanya ufuatiliaji na tathmini katika kipindi cha mwaka 2022 hadi 2023. Hivyo tunaamini kuna vyombo vimeweza kuleta mabadiliko makubwa na vinahitaji kutambuliwa na kuthaminiwa.
Tunzo hii itahusisha kazi zilizotolewa na waaandishi wa habari katika vyombo vya habari vya aina nne (4) kama ifuatavyo:
Uandishi wa habari za Makala katika magazeti (feature articles).
Uandishi wa habari wa vipindi katika redio (radio program).
Uandishi wa habari katika Televisheni (TV program).
Uandishi wa habari wa makala katika mitandao ya kijamii (feature articles in social media story).
Vigezo muhimu vya kuzingatia ni;
∙ Ubora wa kazi iliyowasilishwa.
∙ Upekee wa mada.
∙ Umuhimu wa kuzingatia uwiano sawa wa jinsia.
∙ Vyanzo vingi vya habari vilivyojitawanya.
∙ Ubunifu wa mada husika.
∙ Matokeo baada ya kutoka habari au kipindi hicho (impact).
∙ Uwasilishaji wa mada husika.
∙ Mpangilio wa mada.
∙ Ufasaha na mtiririko wa lugha.
∙ Kuzingatia maadili ya uandishi wa habari.
∙ Uweledi na matumizi ya TAKWIMU.
Kipindi cha Redio na Television kisizidi dakika 30 na pia sauti na picha ziwe katika ubora unaostahiki.
Kipindi au makala iliyochapishwa au kurushwa HEWANI katika vyombo mbali mbali vya habari vikiwemo magazeti, runinga, redio na mitandao ya kijamii katika kipindi cha kuanzia Januari 1 hadi Disemba 31, 2024.
Kama ilivyokuwa kwenye vyombo vya habari SWIL pia ilikaa na waaandishi wa habari 170 kwa mafunzo na majadiliano kuhusu kuandika habari nzuri za wanawake na
@TAMWA_Zanzibar www.tamwaznz.or.tz
uongozi. Kiasi cha waandishi wa habari 45 wametambuliwa kwa kuandika habari za kuongeza ushiriki wa wanawake kuanzia 2021 hadi 2023.
Mchakato wa Uwasilishaji na Vigezo vya Tathmini
Dirisha la kupokea kazi liko wazi kuanzia kwa waandishi wa habari kutoka vyombo vya habari mbalimbali Zanzibar, ikiwemo magazeti, televisheni, redio, na mitandao ya kijamii. Jopo la majaji, likiwa na wataalamu wa uandishi wa habari na utetezi wa kijinsia, litapitia kazi za vyombo vya habari na za waandishi wa habari mapema Januari baada ya kukamilika kwa zoezi la ukusanyaji kazi.
Maombi yamefunguliwa leo na kazi zitaendelea kupokelewa hadi tarehe 5 Januari, 2025. Waandishi wa habari wanaweza kuwasilisha kazi zao ambazo zimezalishwa kuanzia Januari hadi Disemba, 2024 moja kwa moja Ofisi za TAMWA ZNZ zilizopo Tunguu na Mkanjuni Chakechake Pemba, au kupitia barua pepe ya info@tamwaznz.or.tz na kiungo/link itakayotumwa kwenye mitandao ya kijamii.
Hitimisho
Tunawakaribisha waandishi wa habari na vyombo vya habari kushiriki katika tuzo hizi muhimu, ili habari zenu ziwe ushahidi wa nguvu ya uandishi wa habari katika kuleta mabadiliko chanya. Kwa maelezo zaidi, tafadhali wasiliana nasi kupitia info@tamwaznz.or.tz, & ngalapi@tamwaznz.or.tz.
Tuzo hizo ambazo ni mara ya nne kufanyika zinafanywa kupitia mradi wa Kuwajengea Wanawake Uwezo katika Uongozi (SWIL) kwa mashirikiano na Ubalozi wa Norway.
@TAMWA_Zanzibar www.tamwaznz.or.tz