Mkurugenzi wa Operesheni wa Kanda ya Afrika wa kampuni ya michezo ya kubashiri ya LEONBET, Jérôme J. Dufourg (kulia) akizungumza wakati wa uzinduzi rasmi wa kampuni hiyo kwenye ukumbi wa Warehouse Masaki ambao uliopambwa na burudani ya kisasa ya kuvunja mbavu ya wachekeshaji maarufu nchini uliopewa. Uzinduzi huo ulijulikana kwa jina la ‘CHEKA TU: LEONBET EDITION’. Kushoto ni meneja mkuu wa LEONBET Tanzania, Tumaini Maligana
Meneja Mkuu wa kampuni ya michezo ya kubashiri ya LEONBET, Tumaini Maligana (kushoto) akizungumza wakati wa uzinduzi rasmi wa kampuni hiyo uliofanyika kwenye ukumbi wa Warehouse Masaki ambao ulipambwa na burudani ya kisasa ya kuvunja mbavu kutoka kwa wachekeshaji maarufu nchini. Uzinduzi huo uliopewa jina la “CHEKA TU: LEONBET EDITION. Kulia ni Mkurugenzi wa Operesheni wa Kanda ya Afrika wa kampuni ya michezo ya kubashiri ya LEONBET, Jérôme J. Dufourg.
Wachekeshaji maarufu wa “CHEKA TU”, Ndaro ambaye ni balozi wa LEONBET akiwa na Coy Mzungu wakati wa uzinduzi rasmi wa kampuni uliofanyika Novemba 8 kwenye ukumbi wa Warehouse Masaki.
………………
Na Mwandishi wetu
Dar es Salaam. Mashabiki wakubashiri wa kampuni inayotamba ya LEONBET Tanzania walipata burudani ya kisasa ya kuvunja mbavu na wachekeshaji maarufu nchini kwenye uzinduzi rasmi wa kampuni hiyo uliopewa jina la CHEKA TU: LEONBET EDITION.
Burudani hiyo ya kisasa ilifanyika Novemba 8, 2024 kwenye ukumbi wa Warehouse Masaki.
Mashabiki wa vichekesho nchini walipata burudani kutoka kwa wakali wa Cheka Tu, akiwemo Coy Mzungu, Ndaro, Asma, Mtumishi Obama, na Chard Talent, ambao walihakikisha kuwa kila aliyehudhuria anatabasamu na kufurahia uzinduzi huo.
Burudani zaidi zilifuatia kwa muziki wa moja kwa moja kutoka kwa wasanii wakubwa wa Tanzania, akiwemo Maua Sama na Jaivah, ambao walifanya tamasha kuwa la kukumbukwa kwa mashabiki wote.
Katika tukio hilo, Meneja Mkuu wa LEONBET Tumaini Maligana pamoja Mkurugenzi wa Operesheni wa Kanda ya Afrika kwa LEONBET, Jérôme J. Dufourg katika burudani hiyo.
Viongozi hao wakuu wa LEONBET Tanzania waliwashukuru mashabiki wote waliofika katika uzinduzi huo na kuwapa sapoti kubwa.
Maligana, alitoa shukrani za dhati kwa wote waliojitokeza na kwa kuunga mkono uzinduzi wa brand yao.
“Ningependa kuchukua muda mfupi tu kuitambulisha brand yetu ya LEONBET – Simba La Mikeka. LEONBET ni kampuni ya michezo ya ubashiri iliyoingia rasmi Tanzania ili kuambatanisha burudani ya kubashiri kwenye michezo na slots na kutoa fursa ya kutengeneza pesa,” alisema,
Kwa upande wake, Dufourg, akiwakilisha mtazamo wa kimataifa wa LEONBET, alisisitiza dhamira ya kampuni hiyo ya kuleta uzoefu bora wa michezo ya kubashiri kwa Tanzania.
“Tunafuraha sana kuja Tanzania, tukijua kuwa tuna historia na uzoefu wa miaka 15 katika sekta hii, na tunayo dhamira ya kutoa huduma ya kiwango cha juu kwa wateja wetu. Tunaleta si tu ubashiri bali burudani ya hali ya juu kwa wateja wetu nchini Tanzania,” alisema Dufourg.
Dufourg aliendelea kueleza jinsi LEONBET inavyoweka msisitizo mkubwa kwenye huduma bora za wateja.
“Tunataka kuhakikisha kwamba mteja anafurahia uzoefu wake bila tatizo lolote. Kutoka kwa malipo ya haraka, tovuti yenye kasi, hadi bonasi nyingi, tuko hapa ili kurahisisha na kuboresha kila sehemu ya uzoefu wa kubeti na kucheza kasino,” aliongeza.
Maligana na Dufourg walifurahia kuwakilisha LEONBET kama sehemu ya mtindo wa maisha kwa wapenzi wa michezo na burudani.
Maligana, alieleza kuwa, kwa kujiunga na LEONBET, wateja wanaweza kufurahia ofa mbalimbali mara tu wanapojisajili. “Tuna ofa kibao kwa ajili yako ukijiunga na LEONBET. Ukijisajili tu, unapokea ofa ya kipekee!” alisema kwa tabasamu, akiwasihi washiriki kuchangamkia fursa hiyo.
Alisema kuwa uzinduzi wa LEONBET umeacha alama kubwa kwa mashabiki wa vichekesho na wapenzi wa michezo ya kubashiri nchini Tanzania, na kuthibitisha kuwa LEONBET ni zaidi ya kubeti—ni sehemu ya burudani na maisha kwa watanzania wote.