NA BALTAZAR MASHAKA, MUSOMA
KAMANDA wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa waMara, Augustine Magere,amesema mkakati wa kuzuia majanga ni kuwekeza elimukwa wananchi na wafanyabiashara wa vyombo vya usafirishaji wakiwemo wavuvi nawachimbaji madini.
Pia ametahadharisha wamiliki wa vyombo vya usafiriwa majini wazingatiye uwezo wa vyombo,wasibebe mafuta ya petroli na mizigomikubwa na kuchanganya na watu.
Magere ametoa kauli hiyo, leo katika mahojiano na wandishi wa habari kuhusu mbinu na mikakati ya kuzuia majanga katika jamii yakiwemo yamoto na ajali za majini,barabarani na migodini.
Amesema katika kuzuia majanga ya moto,kuzama majinina ajali zingine wamewekeza elimu kwa wananchi,shuleni,taasisi,viwanda nawafanyabiashara wa vyombo vya usafirishaji wakiwemo wavuvi.
Magere amesema wanatoa elimu ya kuzuia majanga kwaasilimia 75 kabla hayajatokea hawapo kuzima moto,hayo ni matokeo yadharura,wanazuia kwa kufanya ukaguzi na kushauri mamlaka husika na kazi yauokozi ni asilimia 25.
“Kipaumbeleni kuwapa elimu wananchi wakielewa wanaweza kuzuia majanga yasitokee(limitionalcontrol),wawe na vifaa vya kuzima moto na utaalamu wa kuvitumia ili kunusurumaisha ya watu hasa majumbani,viwandani na kwenye vyombo vya usafirishaji kamamagari,mitumbwi ama boti zilizogaguliwa,”amesema.
Magere ameeleza kuwa majanga ama matukio ya ajaliza majini na migodini zinasababishwa hasa na jamii ya wavuvi na wachimbaji wamadini kwa sababu ya kufanya kazi kwa mihemko na mazoea bila kuzingatia sheriana usalama wao.
“Matukio ya uokoaji ni makubwa migodini na majinikwa wachimbaji na wavuvi wasiozangatiausalama wao.Migodini wanatumbukia na kufukiwa na vifusi,mashimo na kambawanazotumia kushuka chini shimoni hazikaguliwi na si imara na hawana vifaa vyamawasiliano wala kubaini kama kuna maji shimoni,”amesema.
Kamanda huyo wa Zimamoto na Uokoaji ameshauriwananchi kuchukua tahadhari majini, magari yakiwemo ya kusafirisha mafuta naabiria yawe na vifaa vya kuzima moto na watu wenye utaalamu wakuvitumia,sanduku la huduma ya kwanza,magari yasijaze mafuta katika vituo vyanishati hiyo yakiwa na abiria, wenye magari na mitumbwi wazingatiye ubebajisalama wa abiria.
Kuhusu mitizamo ya wananchi kuwa wanafika katikamatukio bila maji, amesema si sahihi muda wote mtambo wa kuzima moto (gari),unakuana maji ya kutosha na dawa,yakiisha hurejea kujaza maji katika visima (FH)vilivyojengwa katika miji kwa kuzingatiamajengo makubwa.
“Changamoto ni watu kutofahamu namba 114 yadharura, hii inasaidia kuepuka ucheleweshaji wa taarifa ambao husababishazimamoto kuchelewa kufika eneo la tukio kwa wakati ama wengine wana hofu yakutozwa gharama kwa huduma hiyo,ni ya bure,”amesema Magere.
Amewataka wananchi wasisite kutoa taarifa zamajanga kwa maelekezo sahihi na kuwataka watumiaji wa vyombo vya moto wakuachatabia ya kuzuia magari ya wagonjwa na ya kuzima moto,kwani wanacheleweshashughuli za uokoaji.
Pia changamoto ya ujenzi holela inachangia kuzibahasa barabara za mitaa na kusababisha magari ya watoa huduma kushindwakupita,na kushauri wananchi wanapojenga nyumba waache nafasi ya miundombinu yabarabara na kabla wawasilishe michoro ya majengo yao wapate.