Na Mwandishi wetu Geita.
WAKATI
Maonesho ya Saba ya teknolijia ya madini yakiendelea mkoani Geita
kamapuni mbalimbali zinashiriki maonesho hayo zikiwemo zinazosambaza
bidhaa za migodini hasa wauzaji wa magari pamoja na mitambo.
Kwa
mwaka huu kitu cha kipekee ni ushiriki wa shule binafsi katika maonesho
hayo.Miongoni kwa shule hizo ni za Waja na Savannah Plain ambazo
zinatoka kanda ya ziwa pamoja na shule za FEZA
Katika Banda la
Shule ya FEZA huduma wanazozitoa ni pamoja na usahili wa wanafunzi kwa
kidato cha kwanza kwa muhula mpya wa masomo wa 2025
Akizungumza
katika maonesho wakati wanafunzi wa shule mbalimbali za sekondari mkoani
Geita walipotembelewa banda lao kwa lengo la kujifunza Ofisa Mratibu
na Msaili wa wanafunzi wa FEZA ,Huzaifa Sizya amesema wao wamejikita
katika kutoa elimu bora na zeye viwango vya kimataifa kwa shule zenye
mtaala wa Kimataifa (Feza International).
Ameongeza kuwa pamoja
na viwango vya kitaifa chini ya NECT na kusisitiza FEZA imekuwa
ikiongoza katika matokeo ya Kidato cha Nne na Sita kwa miaka yoote
ikijivunia rekodi ya kutoa daraja la kwanza kwa wanafuzi woote miaka
zaidi ya 10 sasa
Pia ameema FEZA iko mbioni kufungua shule kanda
ya ziwa ili kuwaletea wananchi na wazazi huduma jirani na kuunga mkono
juhudi za serikikali kuhakikisha wanafunzi wanapata elimu bora na si
bora elimu.
“FEZA ina mpango wa kuwasomesha bure wanafunzi
ambao wanauwezo wa kimasomo darasani lakini kutokana na changamoto za
familia hawana uwezo wa kusomeshwa, hivyo wanafunzi wenye changamoto
hizo hupata ufadhili hasa wale wenye uwezo mkubwa katika masomo ya
Sayansi ili kutengeneza madaktari na Wahandisi wa kada mbalimbali.”.