Na. Josephine Majura, WF, Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamis Shaaban, kwa niaba ya Katibu Mkuu, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Taasisi ya Wakaguzi wa Ndani Tanzania (IIA), Dkt. Zelia Njeza, katika Ofisi za Wizara ya Fedha, Treasury Square, jijini Dodoma.
Katika kikao hicho wamejadiliana namna bora ya kushirikiana katika kukuza taaluma ya Wakaguzi wa Ndani nchini, ambapo kikao hicho kimehudhuriwa pia na Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali (IAG), Bw. Benjamin Magai na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Wakaguzi wa Ndani Tanzania (IIA), Bw. Seif Hassan na Afisa Mikakati na Maendeleo ya Biashara wa Taasisi hiyo, Bi. Iq-lima Issa.






(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Dodoma)