
Rais wa Jamhuri ya Muunganio wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Dkt Samia Suluhu Hassan, leo tarehe 18 Januari 2025 amefungua Mkutano Mkuu Maalumu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Taifa, leo tarehe 18 Januari, 2025 katika Ukumbi wa Jakaya Mrisho Kikwete Convention Centre, Dodoma, Tanzania.

Akihutubia washiriki wa Mkutano huo ambao ni wajumbe wa CCM kutoka pande mbalimbali za Tanzania, Rais Samia ameainisha mafanikio mbalimbali yaliyotekelezwa na chama hicho katika kipindi cha uongozi wake, na kuwahasa wajumbe na wanachama wa CCM kuwatumikia watanzania kwa weledi na juhudi, huku wakiepuka kufanya kazi kwa makundi; hasa baada ya ukamilifu wa chaguzi za ndani.