Maafisa wa India wameripoti kuwa raia 104 wa nchi hiyo wamefukuzwa kutoka Marekani kwa kutumia ndege ya kijeshi ambapo hatua hiyo inakuja wakati masuala ya uhamiaji kati ya nchi hizo mbili yameendelea kuibua mijadala, huku wengi wa waliofukuzwa wakidaiwa kuingia nchini humo bila vibali halali.
Aidha ripoti zinaeleza kuwa baadhi ya waliorejeshwa walifungwa pingu wakati wa safari yao, hali iliyozua malalamiko kutoka kwa familia na viongozi wa kisiasa nchini India. Wabunge wa upinzani wametaka serikali kutoa maelezo kuhusu madai ya unyanyasaji dhidi ya raia hao wakati wa kurejeshwa kwao
Waziri wa Mambo ya Nje wa India, Subrahmanyam Jaishankar, amesema kuwa serikali inaendelea kushirikiana na Marekani ili kuhakikisha kuwa raia wa India wanaorejeshwa wanaheshimiwa haki zao. Ameeleza kuwa matumizi ya pingu kwa wahamiaji wanaorejeshwa yamekuwa sehemu ya utaratibu wa Marekani tangu mwaka 2012
Tukio hili limeongeza msukumo wa majadiliano kuhusu uhamiaji kati ya India na Marekani, hasa wakati viongozi wa mataifa hayo mawili wanapojiandaa kujadili masuala ya usalama na sera za uhamiaji katika mazungumzo yanayotarajiwa hivi karibuni
The post Raia 400 wa India warudishwa kwao na ndege ya jeshi kutoka Marekani first appeared on Millard Ayo.