Wafanyakazi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Iringa wamefanya bonanza la michezo mbalimbali ikiwa ni kwa lengo la kupongezana kwa kazi, burudani za pamoja za kujiimarisha kiafya.
Bonanza hilo limefanyika February 15, 2025 katika Viwanja vya Samora ambapo jumla ya Watumishi 350 wameshiriki katika michezo mbalimbali kama kuvuta kamba, kukimbia pamoja na mpira wa Miguu.
Akizungumza Mkurugenzi wa TANESCO Kanda ya Magharibi Richard Swai ameitaka Jamii kujenga tabia ya kufanya mazoezi mara kwa mara ili kujiepusha na magonjwa yasioambukizwa.
Kwa Upande wake Meneja wa TANESCO Mkoa wa Iringa Grace Ntungi amesema lengo kubwa la bonanza hilo ni kujenga Umoja na Mshikamano Kwa Wafanyakazi lakini pia kuhimarisha Afya ya akili na mwili jambo ambalo linapelekea kuongeza ufanisi wa utendaji kazi.
Baadhi ya Wafanyakazi wa shirika hilo wamesema uwepo wa michezo hiyo imejenga mahusisno mema baina ya watumishi wa shirika hilo na uongozi wao
The post Watumishi TANESCO waaswa kushiriki michezo first appeared on Millard Ayo.