Mkuu wa mkoa wa Tabora Paul Chacha amemuagiza Katibu Tawala wa mkoa huo kumsimamishwa Meneja wa Wakala wa huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA) mkoa wa Tabora, Mayala Mburi kwa tuhuma za matumizi ya Lugha chafu za matusi kwa wateja.
RC Chacha ametoa maelekezo hayo akiwa Ofisi ya wakala hiyo baada ya yeye pamoja na watumishi kutoka ofisi ya Waziri mkuu kupiga simu kwa nyakati tofauti majira ya usiku kwa lengo la kuhitaji huduma ya mafuta katika kituo cha serikali wakiwa safarini kuelekea mkoa wa Geita na badala yake menehja huyo aliwaporomoshea matusi akidai anapata starehe kwa wakati huo.
“Aliwasiliana yeye mwenyewe na watumishi sita kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu wanaenda kwenye tukio kubwa Geita akawambia mkifika mida ya saa mbili au saa tatu (usiku) mtahudumiwa na bahati mbaya watumishi hao wamefika majira ya saa tatu usiku wakapiga simu kuanzia saa tatu mbaka saa nne simu haijapokelewa badala yake ikaja kupokelewa majira ya saa nne na nusu aliwatukana matuzi ya nguoni huyu bwana anawaambia ninyi ni nani mnanipigia simu usiku huu simu mimi nipo kwenye starehe zangu” Paul Chacha RC Tabora
Kwa mujibu wa maelezo ya mkuu wa mkoa Paul Chacha anasema meneja huyo aliendelea kuwajibu kwenye simu akisema “Aliyekupa mamlaka ya kunipigia simu mimi meneja wa kituo (GPSA) usiku huu niamke niache starehe zangu nije kukuhudumia”
Aidha,katika hatua nyingine Chacha ameagiza kusimamishwa kazi kwa watumishi wawili wa wakala wa Barabara Tanzania mkoa wa Tabora TANROAD Meshack Deogrtius na Godfrey Gration wasimamizi wa kituo cha mizani cha Tuli kwa tuhuma za kupokea Rushwa ambapo imetajwa kuwa siku ya ijumaa ya Tarehe 14 Februari 2025,walikamata gari ambalo mzigo ulikuwa umezidi lakini baadae waliliachia gari hilo baada ya kupokea Rushwa kutoka kwa Mmiliki wa gari hilo.
The post RC Chacha aagiza kumsimamishwa kwa Meneja wa Wakala wa huduma ya Ununuzi Serikalini Tabora first appeared on Millard Ayo.