Na mwandishi Wetu
NAIBU Waziri wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Deus Sangu, amekagua na kufurahishwa na Utekelezaji mkubwa uliofanywa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) Manispaa ya Iringa Kwa kukamilisha Ujenzi wa Daraja muhimu linalotumiwa na Wananchi katika Kata ya Kitwiru ndani ya Manispaa hiyo.
Wananchi wa Kata ya Kitwiru Manispaa ya Iringa wameeleza kuwa hapo awali hasa katika kipindi cha mvua, watoto mpaka watu wazima walikuwa hawawezi kuvuka eneo hilo jambo ambalo lilikuwa linakwamisha shughuli Nyingi za kiuchumi na kupelekea baadhi ya Wananchi kukosa huduma na mahitaji ya Msingi ya Kila siku huku Wanafunzi wakishindwa kwenda Shule na wengine kushindwa kurudi Nyumbani kwasababu njia ilikuwa haipitiki kabisa.
Baada ya Kutembelewa na Naibu Waziri huyo, Wananchi hao wameishukuru TASAF huku wakieleza furaha yao wakisema kuwa kukamilika Kwa Ujenzi wa Daraja hilo ni hatua kubwa ya kimaendeleo kwani Daraja hilo ni mkombozi limefungua Mawasiliano hivyo hawana wasiwasi tena hata ikifika kipindi cha mvua njia hiyo itakuwa inapitika kirahisi na Kila mtu kuanzia Mdogo mpaka mkubwa.
Jambo lililomfurahisha zaidi Naibu Waziri Deus Sangu ni Kusikia kuwa asilimia kubwa ya mahitaji ya Ujenzi wa Daraja hilo kuanzia Mchanga, Kokoto na mawe vimenunuliwa kutoka Kwa Wanufaika wa TASAF ambao Kupitia Vikundi Vyao walikuwa wakifanya Uzalishaji huo kama njia ya kujipatia kipato kuendesha maisha yao ya Kila siku nje ya Pesa wanazopokea kutoka TASAF kusaidia Kata Maskini.