Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akivuta utepe kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa barabara ya Bagamoyo (Makurunge)-Pangani -Tanga (km 256) sehemu ya Mkange-Pangani-Tanga (170.8) pamoja na Daraja la mto Pangani (M525) kwenye hafla iliyofanyika Pangani mkoani Tanga tarehe 26 Februari, 2025.
Muonekano wa Daraja la muda linalotumika kupitisha vifaa kwa ajili ya ujenzi sambamba na ujenzi wa nguzo za Daraja la mto Pangani ukiendelea Wilayani mkoani Tanga, tarehe 26 Februari, 2025.
Shamrashamra za wananchi wa Pangani katika mkutano wa hadhara wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan uliofanyika kwenye uwanja wa kumba ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kikazi mkoani Tanga tarehe 26 Februari, 2025.