Taasisi ya Joel Nanauka Foundation, chini ya Muasisi wake Dkt. Joel Arthur Nanauka, imeendesha zoezi la ugawaji wa kadi za Bima ya Afya kwa Wazee 204 katika Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara-Mikindani.
Zoezi hilo limefanyika katika Kata ya Chuno, Mtaa wa Ligula B, likihudhuriwa na Wazee kutoka maeneo mbalimbali pamoja na Viongozi wa Serikali.
Akiongea wakati wa hafla hiyo, Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara, Gwakisa, amepongeza juhudi za Nanauka Foundation kwa kutambua na kuthamini mchango wa wazee kwa kuwapatia kadi za Bima ya Afya. Pia, amewataka watumishi wa sekta ya afya kuhakikisha wazee wanapata huduma bila vikwazo vyovyote.
Kwa upande wake, Dkt. Joel Nanauka (@joelnanauka_) amesema kuwa Nanauka Foundation imekuwa mstari wa mbele katika kusaidia makundi yenye uhitaji kwa lengo la kuboresha maisha yao, huku akisisitiza kuwa huo ndio utamaduni wa taasisi hiyo katika kuwahudumia Wananchi.
Baadhi ya Wazee waliopokea kadi hizo wametoa shukrani zao kwa taasisi ya Nanauka Foundation, wakisema kuwa hatua hiyo itawasaidia kupata huduma za afya kwa urahisi na bila changamoto kubwa za kifedha “Mimi nimekuwa nikihangaika kupata matibabu kutokana na kukosa uwezo wa kulipia gharama za hospitali, lakini sasa kupitia kadi hii, nina uhakika wa kupata matibabu bila shida,”
The post Nanauka Foundation yakabidhi kadi za bima ya afya kwa wazee 204 Mtwara first appeared on Millard Ayo.