Na Vero, Ignatus Arusha
KWAYA ya Mtakarifu Rita wa Kashia katika Parokia ya Mtakarifu Yuda Tadei jijini Arusha imesema inahitaji kupata Sh.milioni 50 kwa ajili ya kununua vifaa vitakavyosaidia katika kuhubiri na kurahisisha huduma ya Uinjilisti.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa wimbo maalum wa Tawala Bwana,Prof. Joseph Ndunguru ambaye ni Mlezi wa kwaya hiyo amesema malengo yao ni kuhakikisha wanapata kiasi hicho cha fedha ili kununua vifaa.
Aidha Prof. Ndunguru amesema kuwepo kwa vifaa vya kisasa husaidia upanuzi wa wigo wa huduma, uhifadhi wa kumbukumbu, uboreshaji wa ubora wa sauti.Pia inasaidia kuhifadhi historia ya kwaya na kurithisha nyimbo na mila kwa vizazi vijavyo
Ameitaka jamii na waumini kuendelea kuunga mkono jitihada zinazofanywa na kwaya mbalimbali kwa jumbe zinazoimbwa zinaweza kubadilisha maisha ya watu wengine na kuwainua waliovunjika mioyo na kupiga hatua nyingine.
“Tunahitaji kupata kinanda kidogo, spika power mixer, Umplifire, tumba, pamoja na vishkwambi kwaajili ya matumizi ya nota ya nyimbo tunazoziimba Mara kwa Mara kanisani”.
Kwa upande wake Jonas Aloyce Ngowi ambaye ni Mwenyekiti wa kwaya hiyo amesisitiz malengo yao kwa mwaka 2025 ni kukusanya Sh.milioni 50 kwaajili ya akiba ya kwaya kupata vifaa hivyo .
Ngowi amesema kutokuwa na hivyo vifaa kumekuwa na changamoto katika uinjilishaji kwani mara nyingi wanatumia karatasi ambapo zinapotumika au kuloazinachakaa na kupotea
Pia amesema wanaendelea kuuza nyimbo katika flashi kwaajili ya kuongeza kipato cha kwaya kutembelea Parokia na sehemu mbalimbali kwaajili ya kuinjilisha na kufanya mauzo ili kufikia lengo.
Ameongeza kuwa utambulisho wa wimbo huo umekwenda sambamba na uzinduzi wa Rita Charity pamoja na kutambulisha mfumo mpya wa kurekodi nyimbo za Injili.
“Kwaya yetu tunapambana kutoa huduma bora za kuinjilisha,matendo ya huruma ,majitoleo kwa kutumia njia za kisasa zinazogusa watu wa zama hizi bila kuharibu tungo za miziki wala kuharibu tungo za miziki na misingi ya Kikatoliki.”
Katika picha ni kwaya ya Rita wadogo Mtakatifu Rita wa Kashia katika Parokia ya Mtakatifu Yuda Tadei, wakiwa katika muonekano huo wakiimba katika utambulisho wa wimbo maalum wa Tawala Bwana
Prof. Joseph Nduguru Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Arya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA) ambaye pia ni Mlezi wa Mtakatifu Rita wa Kashia katika Parokia ya Mtakatifu Yuda Tadei,
Prof. Joseph Nduguru Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA) ambaye pia ni Mlezi wa Mtakatifu Rita wa Kashia katika Parokia ya Mtakatifu Yuda Tadei, akiwa na Rita Wadogo.