Waziri Mkuu Mstaafu Pinda akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) baada ya kutembelea kwenye kongamano la miaka 30 ya VETA.
Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda akipata maelezo kutoka mhitimu wa VETA ambaye hana mikono akionyesha umahiri wa kuchora kwa kutumia miguu yake katika Maonyesho ya Kongamano la Maadhimisho ya Miaka 30 ya VETA ,jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa VETA CPA Anthony Kasore akiwa katika moja ya banda la Fani Mechatronics kwenye maonesho ya maadhimisho ya miaka 30 ya VETA ,jijini Dar es Salaam.
Matukio katika Picha za Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda akiwa katika mabanda mbalimbali katika maadhimisho ya miaka 30 ya VETA yanayoendelea jijini Dar es Salaam.
*Asema katika kasi hiyo nchi itafika mbali
*CPA Kasore aahidi VETA kuendelea na mabadiliko zaidi na zaidi
Na Chalila Kibuda,Michuzi TV
WAZIRI Mkuu Mstaafu,Mizengo Pinda amesema kuwa kuna mabadiliko ya utoaji mafunzo ya ufundi Stadi kwa vijana na wadau kuonyesha ubunifu katika maendeleo ya Taifa.
Waziri Mkuu Mstaafu Pinda ameyasema katika Kongamano la Maadhimisho ya Miaka 30 ya VETA mara baada ya kutembelea maonesho ya Vyuo vya VETA na Wadau wenye ushirikiano na VETA katika ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNCC) jijini Dar es Salaam.
Amesema kuwa mabadiliko ya utoaji wa mafunzo ya Ufundi Stadi ndio yanachagiza maisha ya kila siku ya mwanadamu kutokana na vitu anavyofanya vinatokana na ufundi.
“VETA ilipofikia na kusema kama tukiendelea hivi na kujiboresha zaidi kiteknolojia basi tutafika mbali na itakuwa ndiyo ukumbozi wa taifa letu”amesema Pinda.
Hata hivyo Amesema kuwa VETA imefanya kazi katika kuwa ushirikiano na wadau wakiwemo Kituo cha Uwekezaji Nchini (TIC) kuwa mwekezaji akiwekeza nguvu kazi ya ufundi wanapata vijana kutoka VETA.
Hata hivyo amesema kuwa kuna mchango unaonekana kwa taifa kutokana na vijana kujiajiri kupitia ujuzi wao waliopata kutoka vyuo vya VETA.
Waziri Mkuu Mstaafu Pinda amepongeza Serikali katika uwekezaji wa ujenzi wa vyuo vya VETA nchi nzima ambayo ni fursa ya vijana kupata mafunzo ya ufundi Stadi na kuwa wazalishaji bidhaa na ufundi kwenye sekta mbalimbali.
Mkurugenzi Mkuu wa VETA CPA Kasore amesema si kwamba, Waziri Mkuu Mstaafu Pinda ni mgeni VETA bali amefika kwenye kongamano kujionea ilipofikia maana akiwa Waziri Mkuu alihusika kusimamia maboresho makubwa yaliyoifikisha VETA hapa ilipofikia.
Amesema kuwa VETA ilipofikia wanaendelea kufanya maboresho ya mifumo kuendana na teknolojia kwa vijana wanapoingia kwenye ajira wanakuwa wamejitosheleza .
Mkurugenzi Mkuu wa VETA, CPA Anthony Kasore amemshukuru Waziri Mkuu Pinda kwa kuweza kufika kwenye kongamano hilo na kujionea kinachoendelea VETA.