Kampuni mashuhuri ya kitalii ya nchini Tanzania ZARA TANZANIA ADVENTURES imetoa mchango wa madawati katika shule ya msingi Kaloleni iliyopo wilayani Moshi Mkoa wa Kilimanjaro.
Mchango huo ni moja ya mafanikio ya hamasisho la kampeni ya Twenzetu Kileleni msimu uliopita wa 2024. Hivyo Zara Tanzania Adventure imeendelea kuwa kinara katika utoaji wa huduma za kitalii nchini Tanzania hususani katika safari za upandaji Mlima Kilimanjaro na safari za Hifadhi za Taifa, kwa wageni mbali mbali wanaofika kutoka mataifa mbalimbali na watalii wa ndani.
Zara Tanzania Adventure, ambayo imeendelea kuwa kinara katika mfululizo wa ushindi wa Tuzo za Utalii Duniani yaani World Travel Awards, sasa Zara imeingika katika kinyang’anyiro hicho tena kwa msimu wa 2025.