Na Kalamu huru ya Leah D. Mbeke
Kutoka: Makao Makuu Dodoma
Kila mmoja wetu amehabarika kupitia vyombo vya habari kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amepokea Tuzo ya Kinara wa Maji Afrika (The Pan-African Water, Sanitation and Hygiene Champion Award) kutoka Taasisi ya WaterAid UK iliyoko nchini Uingereza aliyokabidhiwa na Mkurugenzi wa WaterAid Pan Africa Dkt.
Tanko Yussif Azziko wakati wa hafla ya Kilele cha Wiki ya Maji na Uzinduzi wa Sera ya Taifa ya Maji 2002, Toleo la 2025 katika Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City tarehe 22 Machi 2025, Dar es Salaam.
Kutokana na Uwajibikaji, Utendaji kazi na Usimamizi wa falsafa ya 4R wa Rais Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan, hii sio tuzo pekee ambayo ameipata, tuzo zingine alizowahi kupata ni Tuzo ya Tume ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu, Tuzo ya Heshima ya Pyne Afrika kwa kutambua mchango wake katika kuendelea Sekta ya Utalii Barani Afrika, Tuzo ya ujenzi wa Barabara ya Babacar Ndiaye, Tuzo ya mwongozaji Bora ya Watalii iliyotolewa Taasisi ya Kimataifa ya International Iconic Awards, Tuzo ya CARE Impact Awards for Global Leadership.
CCM wakati wote imekuwa wazi na bayana kuhusu lengo lake la kuona kuwa nchi inaendelea kuwa na usalama wa maji na huduma ya maji safi na salama inazidi kuimarishwa na kuwafikia Zaidi ya asilimia 85 ya wakazi wa Vijijini na Zaidi ya asilimia 95 kwa wakazi wa mijini kama ilivyoainishwa kwenye Ibara ya 100 ya Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu 2020-2025.
Ni ukweli usiopingika kuwa tunashuhudia mafanikio makubwa katika Sekta ya Maji nchini, upatikanaji wa maji, vijijini hadi sasa ni asilimia 83 na mijini asilimia 95 ,Ibara ya 100 ya Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2020 – 2025, imetekelezwa kikamilifu na Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Ikumbukwe kuwa, Maji ni hitaji la msingi na haki ya kila mtu na ni bidhaa ya kiuchumi, hivyo tuna Wajibu wa kulinda, kutunza na kuhifadhi vyanzo vya maji. Pia, tunapaswa kujikumbusha kila wakati kuwa mtekelezaji mkuu wa Sera ya Taifa ya Maji ya Mwaka 2002 Toleo la 2025 iliyozinduliwa na Rais Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan tarehe 22 Machi 2025, Mlimani City Dar es salaam, ni sisi wananchi wenyewe, hivyo tunapaswa kuwa mfano katika kulinda, kutunza vyanzo vya maji bila kusahau kuwa kila tone la maji, lina thamani.
Mwisho, Kutokana na jitihada zilizofanywa na Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Ili kuwa na upatikanaji wa maji endelevu, sisi wananchi hatuna budi kushirikiana na Serikali katika kutunza na kulinda vyanzo vyote vya maji ikiwemo miundombinu ya maji iliyojengwa kwa gharama kubwa na ili kuepusha uharibifu wa miundombinu ya maji.
#Kazi na Utu, Tunasonga mbele
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akipokea Tuzo ya Kinara wa Maji Afrika (The PANAFRICAN Water, Sanitation and Hygiene Champion Award) kutoka Taasisi ya WaterAid UK ya nchini Uingereza aliyokabidhiwa na Mkurugenzi wa WaterAid Pan Africa Dr. Tanko Yussif Azziko wakati wa hafla ya Kilele cha Wiki ya Maji na Uzinduzi wa Sera ya Taifa ya Maji 2002, Toleo la 2025 katika Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City tarehe 22 Machi,2025