Mkurugenzi Mkuu wa VETA CPA Anthony Kasore na Mkurugenzi Mkazi wa Enabel Koenraad Goekint wakionesha hati za Makubaliano kati ya VETA na Enabel.

Mkurugenzi Mkuu wa VETA CPA Anthony Kasore ((katikati) akisaini makubaliano na Mkurugenzi Mkazi wa Enabel Koenraad Goekint kwa ajili ya msaada wa Fedha kwa ajili ya Vyuo vya VETA Mwanza na Tanga.
Mkurugenzi Mkuu wa VETA CPA Anthony Kasore wakibadilishana hati za makubaliano na Mkurugenzi Mkazi wa Enabel Koenraad Goekint kwa ajili ya msaada wa Fedha kwa ajili ya Vyuo vya VETA katika Mikoa ya Mwanza na Tanga.
Na Mwandishi Wetu,
MAMLAKA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) wameingia Makubaliano na Shirika la Maendeleo la Ubelgiji (Enabel) kwa shirika hilo kuongeza msaada wa kwa VETA ili kuwezesha vijana wa Tanzania kupata ujuzi unaoendana na mahitaji ya soko la ajira.
Akizungumza mara baada ya kusaini Makubaliano hayo Mkurugenzi Mkuu wa VETA CPA Anthony Kasore amesema kuwa Enabel kuongeza fedha hizo zinakwenda kuchochea vyuo vya VETA kuendelea kuongeza uwezo kuendeleza vijana katika ujuzi mbalimbali.
CPA Kasore amese a makubaliano ya Enabel kuongeza fedha hizo katika vyuo vya VETA Mwanza na Tanga zenye thamani ya zaidi ya sh. bilioni 2 ambapo fedha hizo zitakuwa kwa ajili Mafunzo pamoja na vifaa.
Amesema kuwa katika fedha hizo zaidi ya Bilioni moja zitatumika katika Mafunzo na zaidi bilioni 1.4 zitatumika katika vifaa vya ajili ya kufundishia pamoja na uboreshaji wa miundombinu kwa kwenda kunufaisha vijana 1000 katika Mikoa ya Mwanza na Tanga katika kuwaandaa kwa ajili ya soko la ajira
Makubaliano hayo yamefanyika chini ya mpango wa mradi wa Inclusive Green and Smart Cities (SASA) unaotekelezwa na Enabel kwa kufadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU).
Kasore amesema kuwa VETA kuwa katika mradi huo ni pamoja kuongeza mafunzo kwa wanawake katika fani mbalimbali ikilinganishwa na ilivyo kwa sasa.
Nae Mkurugenzi Mkazi wa Enabel Koenraad Goekint amesema kuwa makubaliano hayo yanalenga vijana kuwapa ujuzi wa msingi wa Ufundi na ujuzi wa mabadiliko katika ushiriki kikamilifu katika uchumi.
“Tunaamini msaada huu utaimarisha kasi ya vijana kupata ujuzi na hivyo kufungua fursa kwenye uchumi kwao”amesema Goekint
Amesema mradi wa Inclusive Cities unasaidia vyuo vya Mafunzo ya Ufundi Stadi na Sekta binafsi kuchochea ushirikiano na Sekta ya Umma ili kuhakikisha wahitimu wa Mafunzo ya Ufundi wana ujuzi unaohitajika sokoni.