Na Oscar Assenga, TANGA.
MKUU wa Mkoa wa Tanga Balozi Batilda Burian leo ameungana na Waislamu mkoani Tanga kushiriki katika ibadaa ya Eid-alfitr iliyofanyika kwenye Msikiti wa Ijumaa Jijini Tanga huku akiwataka wakazi wa mkoa huo kuendelea kutenda matendo mema.
Dkt Batilda aliyasema hayo mara baada ya kumalizika kwa ibada hiyo ambapo aliwataka waumini kuendelea kutenda matendo mema ambayo walikuwa wakiyafanya katika mfungo wa mwezi mtukufu wa ramadhani pamoja na kuendelea kumuombea Rais Dkt Samia Suluhu Baraka tele na maisha marefu
Alisema wanamshukuru mwenyezi mungu kwa Baraka na wanamuombea Rais Dkt Samia Suluhu kilalaheri na mwenyezi Mungu aendelee kumpa maisha marefu na Baraka tele
“Nimefikisha salamu za Rais Samia Suluhu ambaye anawatakia wote salamu za Eid Mbarak na anawaomba muendele kufurahia na kuendeleza matendo mema ambayo tuliyafanya kwenye mwezi wa ramadhani”Alisema
“ Jana Rais Dkt Samia Suluhu aliweza kutushika mkono wakuu wa mikoa wote na kutoa sadaka ya mbuzi kila kituo na kupelekea kwenye vituo vya watoto yatima ili watoto waliopo kwenye mazingira magumu wawaze kufurahia sikukuu hivyo tunaendelea kumuombea rais kilalaheri na mwenyezi mungu ampe umri na maisha marefu na Baraka tele”Alisema
Hata hivyo alisema kwamba wanaelekea kwenye uchaguzi mkuu hana shaka na wanaamni wana Tanga na watanzania wanamuelewa na kumkubalia hivyo ushindi wa kishindo huku akiwataka waendelee kuwa na ukarimu,utulivu.