Na Mwandishi Wetu
WACHIMBAJI wa madini, wanunuzi pamoja na wadau wa madini wamepongeza serikali kuruhusu mfumo wa mnada wa madini ya vito kwa njia ya mtandao kwani unasaidia kuondoa vishawishi vya rushwa na urasimu wa baadhi ya watendaji kwakuwa umekuwa wazi na wa haki
Kauli za wadau wanazitoa kwenye uzinduzi wa mnada wa kwa njia ya mtandao uliyofanyika jijini Arusha ambayo umeratibiwa na Tume ya Madini pamoja na soko la bidhaa Tanzania kwa njia ya kielekitroniki tmx.
Kwa upande wake Mkurugenzikurugenzi wa Ukaguzi na biashara ya madini, Tume ya Madini CPA.Venance Kasiki ameleza namna ya kuratibu zoezi hilo kwa njia ya kieletroniki
Wakati Ofisa Mtendaji Mkuu wa soko la bidhaa Tanzania kwa njia ya eletroniki tmx CPA. Godfrey Malekano ameainisha manufaa ya mfumo huo kwa mfanyabiashara,mkulima na upande wa Serikali .