Puma Energy Tanzania inaendelea kushirikiana na serikali katika kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia ambapo imeshiriki katika hafla ya Mbio za Mwenge wa Uhuru katika Wilaya ya Chalinze zilizofanyika jana mkoani Pwani.
Mkuu wa Kitengo wa Gesi ya PumaGas Bw. Jeffrey Nasser alikabidhi mitungi ya gesi kwa Mkuu wa Wilaya ya Chalinze Mhe. Shaibu Issa Ndemanga na Kiongozi Mkuu wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2025 ndugu Ismail Ali Ussi.
Hii ni dhamira ya kampuni ya kuendelea kuhakikisha jamii inakua salama na safi kwa kutumia nishati safi ya kupikia.
iongozi mkuu wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa 2025, Bw. Ismail Ussi Ali (kushoto) akipokea msaada wa mitungi ya gesi kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Mauzo PumaGas wa Kampuni ya Puma Energy Tanzania, Jeffrey Nasser (katikati), wakati wa shughuli za Mbio za Mwenge wa Uhuru katika Wilaya ya Chalinze, mkoa wa Pwani. Msaada wa mitungi hiyo inayowalenga mama lishe na baba lishe pamoja na walemavu, ni sehemu ya jitihada za Puma Energy Tanzania kuunga mkono jitihada za serikali katika kuhamasisha matumizi na upatikanaji wa nishati safi ya kupikia kwa uhakika na gharama nafuu nchini kote.
Kiongozi mkuu wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa 2025, Bw. Ismail Ussi Ali akizungumza mara baada ya kupokea msaada wa mitungi ya gesi kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Mauzo PumaGas wa Kampuni ya Puma Energy Tanzania, Jeffrey Nasser (wa kwanza kulia), wakati wa shughuli za Mbio za Mwenge wa Uhuru katika Wilaya ya Chalinze, mkoa wa Pwani.
Kiongozi mkuu wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa 2025, Bw. Ismail Ussi (wa kwanza kushoto) Ali akisikiliza maelezo mara baada ya kupokea msaada wa mitungi ya gesi kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Mauzo PumaGas wa Kampuni ya Puma Energy Tanzania, Jeffrey Nasser (wa kwanza kulia), wakati wa shughuli za Mbio za Mwenge wa Uhuru katika Wilaya ya Chalinze, mkoa wa Pwani.
Wananchi wakifurahia bidhaa ya PumaGas waliyokabidhiwa kwa msaada wa kampuni ya Puma Energy Tanzania, wakati wa shughuli za Mbio za Mwenge wa Uhuru katika Wilaya ya Chalinze, mkoa wa Pwani.