Mhadhiri, Mwandishi wa vitabu na Mchoraji Maarufu wa Chuo Kikuu cha Sultan Quaboos cha nchini Oman, Prof. Ibrahim Noor ameishukuru serikali kuendelea na jitihada za kuitangaza Lugha ya Kiswahili duniani kote na kuwaomba watanzania wote nchini kuendelea kukuza lugha ya Kiswahili ili iendelee kuzungumzwa na watu wengi duniani kote.
Ameyasema hayo leo tarehe 12/04/2025 wakati akiwasili nchini kutokea Mascut kupitia Zanzibar amesema kuwa ni lugha yenye kupendwa na kuzungumzwa na wengi sasa duniani kote na kuwaomba watanzania wote duniani kuendelea kutangaza Lugha ya Kiswahili.
“Lugha hii imekuwa kubwa na kupendwa na watu wengi nchini, hivyo nawaomba wote duniani tuendelee kuunga mkono juhudi za watu waliotangulia kukitangaza Kiswahili na wengine waendelee zaidi” amesema Prof. Noor.
Vilevile, ameipongeza serikali kwa kuanzisha tuzo kwa waandishi bunifu ni kuthamini jitihada za kukuza kiswahili na kuchochea usomaji nchini.
Mkurugenzi Mkuu wa TET, Dkt. Aneth Komba aliongoza mapokezi ya Prof. Noor akiwa sambamba na Mwenyekiti wa Kamati ya Tuzo, Prof. Penina Mlama na watumishi wengine wa TET.
Prof. Noor ni mgeni maalumu atakayeshiriki hafla ya Tuzo ya Taifa ya Mwalimu Nyerere ya Uandishi Bunifu itakayofanyika kesho tarehe 13/04/2024 ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango.
Tuzo hizo zitafanyika kwa mara ya tatu mfululizo ambapo, washindi watakabidhiwa zawadi za pesa taslimu pamoja na vyeti.
Tuzo hizo zitafanyika kwa mara ya tatu mfululizo ambapo, washindi watakabidhiwa zawadi za pesa taslimu pamoja na vyeti.