Na Diana Byera – Bukoba
Mkurugenzi wa Kampeni hiyo, (MSLAC) Ester Msambazi akizungumza na waandishi wa habari mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera amesema huduma hizo ni bure na zinawahusu Wananchi wote wenye matatizo ya kisheria,hata wale wenye mashitaka mahakamani lakini hawana uwezo wa kuwalipa Wanasheria.
“Tumefanya kazi mikoa 23 na mkoa wa 24 ni Tanga, kazi inaendelea sasa kampeni imetua mkoani Kagera ambapo Kila wilaya tutafikia kata 10 kwa siku na vijiji 30, tunatarajia kufikia wananchi asilimia 75 wote wenye migogoro ya ardhi ,mirathi na kila kitu kunufaika na huduma zote za kisheria bure,makundi maalumu kama wazee watahudumiwa haraka,” amesema Msambazi.
Amesema huduma nyingine ambazo zitapatikana ni uandikishaji wa vitambulisho vya taifa pamoja na vyeti vya kuzaliwa huku mamlaka zote zinazohusika na masuala ya kisheria zikitarajia kutoa huduma za haraka ndani ya siku tisa na mawakili ambao watakabidhiwa kesi za wananchi watazishughulikia mahakamani mpaka mwisho.
Pamoja na hayo,nae Mkuu wa Mkoa wa Kagera Fatma Mwassa ametoa wito kwa wananchi wote mkoani Kagera kuhakikisha wanajitokeza kwa wingi kuleta kesi zao hasa migogoro ya ardhi ambayo inahusumbua Mkoa wa Kagera kwa asilimia kubwa.
Aidha kupitia kampeini ya huduma za kisheria amewaagiza wataalam kuhakikisha wanavuna mbinu za kutosha za kitaalam kupitia kampeini hiyo na kuwa kampeini hiyo itakapomalizika wataalam na wakuu wa wilaya wasikilizie kero za wananchi Kila Jumanne na Alhamisi.
Amesema kuwa anaamini wananchi watatumia fursa hiyo muhimu kutafuta suluhu na kuongeza furaha katika maisha yao kupitia kampeini hiyo kwani kesi nyingi zitakuwa zimetatuliwa