NA EMMANUEL MBATILO, MICHUZI TV
Mashindano ya Michezo kwa Vyuo Vikuu Msimu wa Pili kupitia Taasisi ya UNICHAMPIONS kwa kushirikina na CUC yanatarajiwa kufanyika kwa awamu ya pili ambapo yatajumuisha mpira wa miguu, mpira wa kikapu,mpira wa wavu na netboli.
Akizungumza leo Aprili 22,2025 Jijini Dar es salaam wakati wa Uzinduzi wa mashindano hayo,Mwanzilishi wa Mashindano hayo, Elly Fadhili amesema michezo hiyo kwa upande wa Mpira wa miguu itakuwa na timu 24,mpira wa kikapu,wavu na netboli itakuwa na timu 16,ambapo kwa ujumla itachezwa michezo 140 kwa kipindi Cha miezi miwili.
Aidha Fadhili ameeleza kuwa mashindano hayo yatafanyika kwa njia makundi kwa mpira wa miguu ambapo yatakua na timu Tano kwa kila kundi na michezo hiyo itafanyika kikanda ambapo vyuo vipo.
” Tumegawanya makundi kutokana na timu hizi amabapo zipo wilaya ya Ubungo watatumia viwanja vya chuo cha Ustawi,ambazo zipo upande wa UDSM zitatumia uwanja wa UDSM na ambazo zipo upande wa Temeke vitatia uwanja wa DUCE Sambamba na timu zilizopo posta zitatumia uwanja wa Muhimbili.”
Aidha amesema katika mashindano ya michezo hiyo kwenye upande wa Mpira wa wavu na kikapu yenyewe itanzia katika hatua ya 16 bora.
Kwa upande wake, Mdau wa Creative UniConect(CUC) Festo Nkuba amesema wameamua kuungana na Unichampions ili kuibua vipaji sio kwenye michezo pekee hata katika talanta nyingine ili kuendeleza walichonacho ili kuwajengea misingi imara katika vipaji vyao.
Amesema wameamua kuwezesha vipaji ambavyo vipo ili kuwawawekea jukwaa washiriki kuonesha vipaji vyao ambapo kuna washiriki katika upande wa ushairi,mziki wa Hip hop ,mitindo ya mavazi pamoja na wacheza mziki.
Amesema katika upande wa shindano la vipaji wanatarajia kuanza mchujo utakaofanyika kwa siku mbili kuanzia Mei 07-08,2025.
Naye, Samndi Abdul Mratibu wa Michezo ya Game ameeleza kuwa miongoni mwamichezo ya game watakayokuwa nayo ni pamoja na Fifa 2025,Checkers,chess,Table Tennis na Pool table wanatarajia kuifanya njia ya makundi ili kupunguza idadi kubwa ya watu ili kupata washindi watatu ambapo mashindano yatafanyika Kila Jumamosi na Jumatano katika kiwanja cha Gwambina lounge na Nafrine Hotel.

Vilevile,Wadhamini wa Mashindano hayo Taasisi ya Mega we Care, James Chisewe amewaalika WANAFUNZI wote kujiunga na Unichampions ambapo litakua jukwaa la kuwainua kuzifikia ndoto zao,ambapo ameeleza kuwa wapo tayari kushirikina na wale watakaofanya vizuri baadae
Aidha amesisitiza kuwa wapo tayari muda wote kwaajili ya huduma ya kwanza ili kuondoa maumivu kwa wanamichezo wote katika kipindi chote Cha michezo.
Pia, Mwanakamati wa Tuzo za Kijamii amesema wameanzisha tuzo za kijamii ambazo zitafanyika kwa wanafunzi ambao wapo katika pande zote za Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ili kutambua uwezo walionao vijana hao.
Aidha amesema watakua na vipengele mbalimbali katika tuzo hizo ambavyo ni uongozi,ubunifu,uigizaji,uwasilishaj, upigaji picha,uandishi,ushawishi wa kijamii ujasiriamali,uwasilishaji wa hadhara,pamoja na uaandaji wa maudhui ambapo washindi watakua wawili katika Kila kipengele kwa kuzingatia jinsia zote mbili.
Michezo hiyo inatarajiwa kulindima kuanzia Tarehe 3,Mei hadi 27June ambapo itakua tamati wa mashindano hayo,Vyuo 24 katika Mkoa wa Dar es salaam vinatarajiwa kushiriki katika mashindano hayo .