Mfuko wa Maendeleo ya Mitaji wa Umoja wa Mataifa (UNCDF) pamoja na washirika wake wa maendeleo wameandaa warsha ya kitaifa ya siku tatu yenye lengo la kuimarisha ushirikiano wa wadau na kuongeza uelewa na uwezo wa jinsi kuainisha vipaumbele vya kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi katika Awamu ya Pili ya utekelezaji wa program ya LoCAL nchini Tanzania.
Washirika wa maendeleo wa UNCDF ni Ubalozi wa Norway nchini Tanzania, Ubalozi wa Ubelgiji nchini Tanzania, Umoja wa Ulaya, na Ubalozi wa Ireland nchini Tanzania.
Akizungumza kwemye warsha hiyo Mratibu wa mradi wa Mabadiliko ya tabianchi wa UNCDF- LoCAL, Aine Mushi amesema lengo la warsha hiyo ni kuimarisha uelewa na uwezo wa kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi na uhimilivu kwa mendeleo endelevu nchini Tanzania.
Pia amesema warsha hii imewakutanisha wadau mbalimbali wanaoshughulika na jitihada mbali mbali za kuweza kupambana na athari za mabadiliko ya Tabianchi zikiwemo taasisi za Serikali, washirika wa maendeleo, Mamlaka za Serikali za Mitaa (LGA), washauri waelekezi na taasisi za elimu ya juu za utafiti ambapo washiriki 80 wamehudhuria warsha hiyo.
“Tunawajengea uwezo kuhusu mpango wa LoCAL kama jukwaa la kuendeleza harakati za kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi na uwezo wa kupanga vipaumbele na kuingiza vifungu kwenye bajeti ya Mamlaka za Serikali za Mitaa ili kujenga uhimilivu wa mabdiliko ya tabianchi kwa wananchi kwa kutumia mbinu shirikishi na zinazozingatia usawa wa kijinsia.” Alisema Mushi

Afisa Misitu Mkuu kutoka Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Ofisi ya Rais – TAMISEMI) Rogacian Lukoa akizungumza kuhusu namna serikali ilivyojipanga kushirikiana na wadau wa maendeleo ili kuweza kukabiliana na mabadiriko ya Tabianchi.
Mshauri wa Kanda wa Mrasi wa LoCAL – UNCDF Jenifer Bukokhe Wakhungu akizungumza kuhusus namna shirika hilo lilivojipanga kuendelea kutoa mafunzo mbalimbali ili kuongeza uwezo wa serikali , halmashauri na vijiji kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi hapa nchini.
Afisa Mazingira Mkuu kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais(VPO) Mhandisi Mwanasha Rajabu Tumbo akitoa salamu za ofisi hiyo wakati wa warsha ya kitaifa kwa lengo la kuimarisha ushirikiano wa wadau na kuongeza uelewa na uwezo wa jinsi kuainisha vipaumbele vya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi katika Awamu ya Pili ya utekelezaji wa program ya LoCAL nchini Tanzania.
Mkuu wa Ushirikiano na Maendeleo kutoka Ubalozi wa Ubeligiji nchini Tanzania Fanny Heylen akizungumzia ushirikiano wa Ubalozi huo na Mfuko wa Maendeleo ya Mitaji wa Umoja wa Mataifa(UNCDF).
Mshauri Mwandamizi wa Kilimo, Mabadiliko ya Tabianchi, na Utafiti kutoka Ubalozi wa Norway, Bw. Yassin Mkwizu akitoa salamu za ubalozi huo kwa wadau mbalimbali kwenye warsha iliyoandaliwa na Mfuko wa Maendeleo ya Mitaji wa Umoja wa Mataifa(UNCDF) pamoja na washirika wake.
Mratibu wa mradi wa Mabadiliko ya Tabianchi wa UNCDF- LoCAL, Aine Mushi akiwasirisha mada kwa wadau mbalimbali kutoka taasisi za Serikali, washirika wa maendeleo, Mamlaka za Serikali za Mitaa (LGA), washauri waelekezi na taasisi za elimu ya juu za utafiti wakati wa warsha hiyo.
Baadhi ya wadau mbalimbali kutoka taasisi za Serikali, washirika wa maendeleo, Mamlaka za Serikali za Mitaa (LGA), washauri waelekezi na taasisi za elimu ya juu za utafiti wakifuatilia mada kwenye warsha hiyo.
Picha za pamoja