NA VICTOR MASANGU, KIBAHA
Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjni Mhe: Silvestry Koka ameweza kutekeleza ilani ya chama cha mapinduzi (CCM) kwa vitendo kwa kipindi cha kuanzia mwaka 2020 hadi 2025 katika nyanja mbali mbali ikiwemo katika sekta ya elimu, afya, maji, pamoja na kuboresha miundombinu ya barabara
Koka akizungumza katika mkutano mkuu maalumu wa Jimbo kwa ajili ya utekelezaji wa Ilani kwa kipindi cha mwaka 2020 hadi 2025 amebainishwa kwamba ameweza kushirikiana na serikali katika kuboresha sekta ya elimu ikiwa pamoja na kuhakikisha kwamba anaboresha miundombinu kwa ajili ya ujenzi wa madarasa mbali mbali.
Amesema kwamba katika kipindi cha miaka mitano ameweza kupambana kwa hali na mali katika kuboresha sekta ya elimu ya msingi ambapo jumla ya shule zipatazo 9 za msingi zimejengwa kwa gharama ya zaidi ya bilioni 2.4 lengo ikiwa ni kuboresha sekta ya elimu kwa wanafunzi wa shule za msingi.
Amebainisha kwamba shule ambazo zimeweza kujengwa ni pamoja naa shule ya Muheza,(Mailimoja) shule ya msingi Mkoleni iliyopo kata ya Mbwawa, shule ya misingi Madina iliyopo kata ya Msangani, shule ya msingi Zegereni iliyopo kata ya Visiga, shule ya msingi Sofu , shule ya msingi Amani, iliyopo kata ya Kongowe,shule ya msingi Kanesa iliyopo kata ya Kongowe, shile ya msingi Saini iliyopo kata ya Visiga, pamoja na shule ya msingoi Mtakuja iliyopo kata ya Pangani.
Aidha Koka amebainisha kwamba serikali kwa kipindi cha mwaka 2020 hadi 2025 imeweza kutoa fedha ambazo zimeweza kwenda kukarabati madarasa 62 katika shule mbali mbali zilizopo katika Jimbo la Kibaha mjini ambapo madarasa hayo yameweza kuwa katika mazingira mazuri na kuwapa wanafunzi kuweza kusoma katika hali ya utulivu.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Nickson John ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mkutano huo maalumu amesema kwamba serikali ya awamu ya sita imetenga fedha nyingi ambazo zimeweza kwenda kusaidia katika utekelezaji wa miradi mbali mbali katika Jimbo la Kibaha mjini ikiwemo mradi mkubwa wa maji katika kata ya Pangani.
Aidha amempongeza kwa dhati Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvstry Koka kuweza kutekeelza ilani ya chama kwa vitendo na kuwatumikia wananchi katika kutatua changamoto zao na kuwaletea chachu ya maendeleo.
Naye Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kibaha mjini Mwalimu Mwajuma Nyamka amesema kwamba katika kipindi cha miaka mitano Mbunge Koka ameweza kushirikiana bega kwa bega na serikali pamoja na wananchi katika kutekeleza ilani kwa vitendo katika suala zima la utekeelzaji wa ilani.
Mkutano mkuu maalumu wa Jimbo kwa ajili ya utekelezaji wa Ilani kwa kipindi cha mwaka 2020 hadi 2025 umewashirikisha wajumbe mbali mbali kutoka kata tatu ikiwemo Kata ya Mbwawa, Visiga, pamoja na Misugusugu.