IKIWA leo hii ni tarehe 28 ya mwezi April, Meridianbet imeendelea na zoezi lake la ufanyaji wa CSR, kurejesha kwenye jamii kile kidogo wanachokipata kwani wanaamini kuwa wenye mahitaji ni wengi. Na safari hii waliamua kutoa vifaa vya michezo kwa timu za wanawake.
Kwanza kabisa katika kuendeleza sekta ya michezo Meridianbet waliona ni vyema kabisa kutoa jezi kwa timu za Mtoni Queens pamoja na Sabasaba Queens ambazo timu hizi zinapatikana katika Kata ya Mtoni jijini Dar es salaam.
Michezo siku hizi imekuwa ni ajira si kwa wanaume peke yake bali hata kwa wanaume katika miaka ya hivi karibuni, ambapo wasichana nao wameamua kujikita kwenye michezo hasa mpira wa miguu.
Ukiachana na Meridianbet kutoa jezi hizo, pia unaweza ukabashiri hapa hapa na kuibuka bingwa sasa. Suka jamvi lako la ushindi leo na ubashiri hapa. Pia cheza michezo ya Kasino ya mtandaoni kama vile, Aviator, Keno, Poker, Roullette, Keno, na mingine kibao.
Basi katika kuunga mkono suala hili la michezo wakali wa ubashiri Tanzania, Meridianbet walitoa jezi kwa timu hizo mbili ambazo zitawasaidia kwenye mazoezi na wakati wa mechi mbalimbali za mashindano ambayo hushindana.
Akizungumza katika hafla hiyo, mwakilishi wa Meridianbet alisema, “Sisi Meridianbet tunaamini kuwa michezo ni jukwaa muhimu sana kwa maendeleo ya vijana na jamii kwa ujumla. Kupitia michezo, vijana wanaweza kujifunza nidhamu, kujituma na kufanya kazi kwa pamoja. Tunajivunia kuwa sehemu ya safari ya mafanikio ya Mtoni Queens na Mtoni Sabasaba.”
Baada ya kupokea jezi hizo viongozi wa timu za Mtoni Queens pamoja na Sabasaba Queens walitoa shukrani zao za dhati kwa Meridianbet kwa msaada wa jezi hizo kwnai hiyo inawapa wao motisha na nguvu ya kupambana zaidi kwenye mashindano yao.
Meridianbet inaendelea kuwa mdau mkubwa wa michezo nchini Tanzania, si tu katika ngazi ya kitaifa bali pia kwenye maendeleo ya michezo katika ngazi ya jamii. Kampuni hii imejikita katika kusaidia vijana kufikia ndoto zao kupitia msaada wa vifaa, udhamini wa mashindano, na programu za maendeleo ya michezo.
Kwa msaada kama huu, Meridianbet inathibitisha kwa vitendo kuwa inayo nia ya dhati ya kuwekeza katika mustakabali wa michezo nchini, na kuwapa vijana fursa ya kuonesha vipaji vyao duniani.